Mapato ya mwaka 2025/26 ya shirika la taifa la Ethiopian Airlines yameongezeka kwa 20% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliotangulia hadi $9.1 bilioni, shirika la Habari la taifa la Ethiopia lilisema siku ya Jumatano.
Shirika hilo la ndege, ambalo ni kubwa barani Afrika, linasema idadi ya abiria imeongezeka kwa 10% hadi milioni 20.7 katika mwaka wake wa fedha hadi Julai 7.
Kusafirisha mizigo kuliongezeka kwa 16% kwa mwaka hadi tani 897,000.
Ethiopian Airlines, ambalo lina ndege zaidi ya 150, lilisema mwezi Aprili kuwa litanunua ndege zingine 6 aina ya Boeing 787-9 Dreamliner.
Mwezi Juni shirika hilo lilisema kuwa litaamua katika kipindi cha miezi mitatu kuhusu kuagiza ndege ndogo za biashara 25 kwa ajili ya safari za ndani.
Shirika hillo liliongeza ndege tisa kipindi hicho, shirika hilo la habari lilisema, likiongeza kuwa eneo lake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole wa Addis Ababa limepanuliwa.



















