| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Kenya: Sumu chanzo cha vifo vya tembo wa Amboseli
Hata hivyo, mamlaka hiyo haikuwewa wazi aliyehusika na kuwapa sumu wanyama hao ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini humo.
Kenya: Sumu chanzo cha vifo vya tembo wa Amboseli
Shirika hilo, lilitadhaharisha kuwa huenda wanyama wafugwao katika eneo lililo karibu na hifadhi hiyo, pia wakaathirika na sumu hiyo.

Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori la Kenya (KWS) limethibitisha kuwa, tembo 15 walikufa kwa sumu iliyokuwa imewekwa kwenye nyanya shambani.

Hata hivyo, mamlaka hiyo haikuwewa wazi aliyehusika na kuwapa sumu wanyama hao ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini humo.

Akizungumza Julai 29, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa KWS, Erustus Kanga alisema kuwa, vipimo vilionesha kuwa wanyama hao walikuwa wamepewa sumu aina ya Sianidi,  kemikali yenye sumu yenye kusababisha kifo, kwa kuzuia seli za mwili kutumia oksijeni.

Shirika hilo, lilitadhaharisha kuwa huenda wanyama wafugwao katika eneo lililo karibu na hifadhi hiyo, pia wakaathirika na sumu hiyo.

Hata hivyo, kulingana na KWS, sumu hiyo haina madhara ya moja kwa moja kwa binadamu.

Hifadhi hiyo, inapakana na jamii zenye kujishughulisha na kilimo na ufugaji.

CHANZO:AP