| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Raia wa Australia akamatwa kwa kufuga mende zaidi ya laki moja
Mamlaka ya kulindawanyamapori imegundua operesheni haramu ya ufugaji wa wadudu iliyokuwa ikiendeshwa kwa ajili ya biashara ya magendo, yenye thamani inayokadiriwa kufikia Dola za Marekani 140,000.
Raia wa Australia akamatwa kwa kufuga mende zaidi ya laki moja
Picha hii inaonyesha mende wa Madagascar walionaswa kutoka kwa mfugaji wa wadudu huko Bathurst, Australia, Jumanne, Mei 26, 2026. / / User Upload

Maafisa wa wanyamapori nchini Australia wamegundua operesheni haramu ya ufugaji wa mende katika jimbo la New South Wales, na kukamata zaidi ya wadudu 100,000 waliokuwa na thamani ya takriban dola za Marekani 140,000 katika soko haramu.

Maafisa hao wameonya kuhusu ongezeko la tishio linalotokana na biashara haramu ya wadudu hao wenye kuenea na kuathiri mazingira asili.

Msako huo ulifanyika katika kituo cha kibiashara cha ufugaji mjini Bathurst, magharibi mwa Sydney, ambapo maafisa walikuta idadi kubwa ya mende aina ya Madagascar na mende wa aina ya Dubia, ambao ni marufuku kufugwa nchini humo, kwa mujibu wa idara ya mazingira ya Australia.

Mende wa Madagascar wanajulikana kwa kutoa sauti ya kipekee kama njia ya kujilinda, huku mende aina ya Dubia wakifugwa mara nyingi kama chakula cha wanyama wanaotambaa, lakini nchini Australia wanachukuliwa kuwa wadudu wanaoweza kuenea na kuathiri mazingira ya asili.

Mamlaka hio imesema ukubwa wa operesheni hiyo unaonyesha ongezeko la wasiwasi kuhusu biashara haramu ya wadudu hatari wanaoweza kuathiri kwa mifumo ya kipekee ya ikolojia ya Australia.

Mamlaka yaonya kuhusu kuongezeka kwa biashara haramu ya wadudu

Maafisa walisema ukamataji huo unatoa ujumbe wazi kwa wafugaji, biashara za wanyama wa kufugwa, na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya spishi zilizopigwa marufuku.

“Tunalichukulia kwa uzito mkubwa jukumu letu la kulinda bioanuwai ya kipekee ya Australia, pamoja na ukiukaji wa sheria za kitaifa za mazingira,” alisema msemaji wa idara ya mazingira, akiongeza kuwa mamlaka zinaona ongezeko la ufugaji na biashara haramu ya mende.

Picha zilizotolewa na maafisa zilionyesha kuwa baadhi ya mende wa aina ya Madagascar waliokamatwa walikuwa wakubwa kiasi cha karibu kufunika kiganja cha mkono wa mtu mzima.

Wadudu hao sasa wataangamizwa kwa njia maalumu, na hivyo kukomesha operesheni hiyo kubwa ambayo mamlaka zinasema ingeweza kusababisha hatari za kimazingira ikiwa spishi hizo zingetoroka au kuenea porini.

 

CHANZO:TRT World and Agencies