| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki na Poland zaazimia kukuza ushirikiano
Mataifa hayo mawili yameazimia kushirikiana katika nyanja ya usalama na biashara, huku maandalizi ya mkutano wa NATO yakiendelea kushika kasi.
Uturuki na Poland zaazimia kukuza ushirikiano
Kulingana na Erdogan, Uturuki na Poland ni washirika muhimu ndani ya NATO./Picha:AA / Others

Uturuki na Poland zinaendelea kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja za ulinzi na usalama, kama washirika wawili wa NATO, amesema Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki.

Akiwa ameambatana na kiongozi mwenzake kutoka Poland Karol Nawrocki wakati wa mkutano na wanahabari jijini Ankara siku ya Jumanne, Erdogan alisema kuwa nchi hizo mbili zinaendelea kushirikiana kuongeza uwezo wao wa kujilinda.

Ulinzi na usalama waangaziwa

Kulingana na Erdogan, Uturuki na Poland ni washirika muhimu ndani ya NATO, akiongeza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo unazidi kuwa muhimu wakati changamoto za kiulimwengu zikiendelea.

Alibainisha kuwa maandalizi ya mkutano wa NATO yalikuwa ni kati ya mambo yaliyojadiliwa na viongozi hao.

Ujazo wa biashara kuongezeka hadi Dola bilioni 15

Hali kadhalika, kiongozi huyo wa Uturuki aligusia ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, akiongeza kuwa ujazo wa biashara umekuwa na kufikia Dola bilioni 15 kutoka Dola bilioni 10.

Erdogan alisema Uturuki ipo tayari kukuza uhusiano na Umoja wa Ulaya kwa maslahi ya pande mbili na kuishukuru Poland kwa kuunga mkono azma ya Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Akizungumzia masuala ya kikanda, Erdogan alisema kuwa anategemea kuona Poland ikiunga mkono mpango wa mataifa mawili kama suluhu ya mgogoro wa Palestina.

Kwa upande wake, Nawrocki alitoa uhakika wa kushiriki mkutano wa NATO, akiipongeza Uturuki kwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

CHANZO:TRT World and Agencies