Rais wa Kenya William Ruto amewasili nchini Tanzania ambapo atafanya ziara rasmi ya siku mbili. Rais Ruto, amepokelewa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan katika ikulu ya Dar es Salaam.
ZILIZOPENDEKEZWA
Viongozi hao wawili wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana, ambapo mambo kadhaa yatajadiliwa. Miongoni mwao, ni pamoja na ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi.
Katika ziara hiyo, Rais Ruto pia anatarajiwa kuhudhuria Jukwaa la Wafanyabiashara, na hatimae kulihutubia Bunge la nchi hiyo huko jijini Dodoma, katikati mwa Tanzania.
CHANZO:TRT Afrika Swahili









