Mazishi ya aliyekuwa waziri wa ulinzi a Mali, Sadio Camara yamefanyika leo jijini Bamako.
Mazishi hayo, yamehudhuriwa na maelfu ya watu, akiwemo kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo, Assimi Goita.
Akiwa amevalia mavazi ya kijeshi, Goita alimmwagia sifa Camara, huku akiwa ameliinamia jeneza lake lililofunikwa kwa bendera ya Mali pamoja na kofia ya kijeshi juu yake.
ZILIZOPENDEKEZWA
Jenerali Camara alipoteza maisha siku ya Jumamosi katika shambulio la bomu lililotegwa ndani ya gari katika eneo lake la makazi karibu na mji wa Bamako.
Serikali ya Mali imetangaza siku mbili za maombolezo kufutia kifo hicho.
CHANZO:AFP













