Shambulio hilo lililotokea Jumatano lilidaiwa kutekelezwa na kundi la kigaidi linalohusishwa na Al-Qaeda, kundi hilo lilisema ya kuwa “limechukua udhibiti wa kituo cha kijeshi cha wapiganaji wa Burkina,” bila kutoa maelezo zaidi.
“Jana majira ya saa saba mchana (1500 GMT) magaidi wenye silaha nzito waliokuwa kwenye pikipiki walifanya shambulio katika mji wa Bagare,” mkazi mmoja wa eneo hilo katika mkoa wa kaskazini wa Passore alisema.
“Milio ya risasi iliendelea kwa zaidi ya saa moja na magaidi walichoma moto makumi ya maduka, magari na pikipiki,” aliongeza.
‘Mashambulizi ya kujihami yafanikiwa dhidi ya adui’
“Hasara ni mkubwa lakini hasa tunaomboleza vifo vya wanachama wa VDP, ambao walilengwa moja kwa moja na washambuliaji,” mkazi mwingine alisema, akimaanisha Volunteers for the Defence of the Homeland (Wajitolea wa Kulinda Nchi).
Chanzo cha usalama cha kikanda kilithibitisha shambulio hilo kwa shirika la habari la AFP, kikisema: “Kituo cha VDP kililengwa na magaidi lakini shambulio la kujihami lilifanikiwa kuwafurusha maadui.”
Mkazi mmoja alisema watu kutoka vijiji vya jirani walikuwa wamekimbilia Bagare kabla ya kushambuliwa siku ya Jumatano.
Burkina Faso yaimarisha usalama
Siku ya Jumanne, serikali ilianzisha operesheni ya kijeshi yenye lengo la kuimarisha usalama kote nchini Burkina Faso.
Pia iliimarisha ulinzi katika mji mkuu, Ouagadougou.
Hatua hizo zilichukuliwa baada ya magaidi na waasi wanaoongozwa na Tuareg kufanya mashambulizi yaliyoratibiwa katika nchi jirani ya Mali.











