| Swahili
Maoni
AFRIKA
4 dk kusoma
Kwa nini Uganda wanatakiwa kutafakari kuhusu mpango wao wa kupeleka vikosi Gaza
Uganda imeahidi kupeleka maafisa wa usalama 1,200 katika mpango uliopendekezwa wa wanajeshi 20,000, kikosi kitakachoongozwa na kamanda wa Marekani Meja Jenerali Jasper Jeffers.
Kwa nini Uganda wanatakiwa kutafakari kuhusu mpango wao wa kupeleka vikosi Gaza
Tarehe 6 Agosti 2026.Bunge la Uganda lilipiga kura ya kuidhinisha kupelekwa kwa wanajeshi 1,200 Gaza. Picha: AA / Anadolu Agency

Na Asuman Kayingi

Mikakati ya Uganda kujihusisha kwenye pendekezo la kuchangia wanajeshi katika Mpango wa Vikosi vya Kimataifa vya Kulinda Usalama (ISF) inaenda kwa haraka. Uhakika wa Kimkakati, kisheria na operesheni unaonesha kuwa mpango huo wa Uganda bado haujathibitishwa wakati Bunge la Uganda lilipopiga kura kuidhinisha vikosi hivyo tarehe 6 Agosti 2026.

Waziri wa Ulinzi wa Uganda Kiryowa Kiwanuka aliwaeleza wabunge kuwa Rais wa Marekani Donald Trump, ametuma wajumbe, kuzungumza na Rais Yoweri Museveni mwezi Julai akitaka Uganda kuchangia wanajeshi katika mpango wa vikosi uliopendekezwa. Uganda imeahidi kupeleka maafisa wa usalama karibu 1,200 katika mpango uliopendekezwa wa wanajeshi 20,000, kikosi kitakachoongozwa na kamanda wa Marekani Meja Jenerali Jasper Jeffers.

La msingi, maafisa wa Jeshi la Uganda pia walisafiri nchini Israel kujadili suala hilo. Iliripotiwa kuwa tarehe 17 Agosti, Maafisa wa kijeshi wa Uganda na Burundi walikuwa ziarani nchini Israel katika kamandi ya jeshi la Marekani huko Kiryat Gat, kwa lengo la kujadili ushiriki wao.

Hali hii inaonesha kuendelezwa kwa mipango ya operesheni hiyo. Pia kuna suala muhimu la kikatiba: Kuidhinisha kwa bunge tarehe 6 Agosti kunaweza kuonekana kama ndiyo mwisho wa uwajibikaji wa bunge wakati baadhi ya masuala ya vikosi hivyo yanajadiliwa?

Naamini jawabu litakuwa siyo.

Kuidhinishwa na bunge kunatakiwa kuwe mwanzo wa kuwajibisha mihimili, siyo mwisho wake.

Mfano yaliyotokea Somalia 2007

Kwa namna bunge la Uganda lilivyoshughulikia kujumuishwa kwa vikosi vyake AMISOM Februari 2007 ni jambo la kupigiwa mfano.

Wakati serikali ilipokuwa inatafuta kuungwa mkono kwa kupeleka vikosi 1,500 vya Uganda nchini Somalia, bunge liliwawajibisha kuhusu pendekezo hilo. Rekodi za bunge zinaonesha kuwa wabunge walihoji kuhusu sheria ya mpango huo, utaratibu wa usimamizi, maslahi ya wanajeshi, mipango ya kifedha na masuala mengine kuhusu vikosi hivyo.

Hatimaye bunge lilipiga kura 155 kuidhinisha mpango huo.

Hata hivyo, kura hiyo, haitakiwi kuonekana kama bunge zima limeunga mkono. Idadi hii ni kwa wale walioshiriki kwenye uchaguzi huo kuliko bunge lote.

Jambo muhimu ni kuwa inakwenda kitaasisi. Kupelekwa Somalia kwa wanajeshi kulitathminiwa kwa muktadha wa kikosi cha kulinda amani cha Afrika kwa lengo la kuhakikisha usalama. Bunge halikuwa linaidhinisha tu mpango wa kisiasa; lilikuwa linatathmini matokeo ya kupeleka majeshi ya Uganda katika mazingira ya vita Afrika.

Hilo ni jambo muhimu la kujifunza.

Maswali lazima yajibiwe

Kabla ya mwanajeshi hata mmoja wa Uganda kupelekwa, Bunge lazima litoe majibu kwa angalau masuala matano muhimu.

Sheria za ushirikiano: Sheria gani ziwaongoza wanajeshi hao? Nini kifanyike wakati wanajeshi wa UPDF wanapokutana na vikosi vya Israel vinapokuwa vinafanya operesheni huru katika eneo lao?

Kuheshimu uongozi: Nani mwenye mamlaka juu ya wanajeshi wa Uganda? Kamanda wa Uganda anaweza kuwa na mamlaka ya kupinga uongozi wa Marekani kama amri itahitalifiana na sheria ya kimataifa ya ubinadamu, sheria ya Uganda au sera ya kitaifa ya Uganda?

Uzingatiaji wa sheria: Utaratibu wa Makubaliano wa Jeshi hilo ni upi? Wanajeshi wa Uganda wanazingatia amri gani wanaposhutumumiwa kwa uhalifu? Utaratibu ni upi iwapo mtu anakamatwa, jeraha au kifo?

Masuala ya Fedha: Nani analipia wanajeshi hao? Vipi kuhusu kulipwa? Silaha gani, bima, na matibabu?

Maslahi ya Kitaifa: Ni faida gani ambayo Uganda inapata katika hilo? Nchi hii inazingatia amani ya kweli Gaza, au ni kuweka maisha ya wanajeshi hatarini na uhalali wa kidiplomasia ili kupata utashi wa kisiasa wa Marekani?

Bunge litathmini upya — siyo kukwepa

Sifa ya vikosi vya kulinda amani vya Uganda ni fahari kwa taifa. Ujasiri na utaalamu wa wanajeshi wa Uganda nchini Somalia na kwingineko hautakiwi, hata hivyo, kuwa suala la kukwepa uwajibikaji.

Ujasiri wa jeshi hauondoi uwazi wa sera ya mambo ya nje.

Swali siyo kama wanajeshi wa Uganda siyo majasiri kwenda Gaza.

Swali muhimu ni kama uongozi wa kisiasa umekuwa wazi zaidi kuhusu kile wanachotakiwa kufanya, chini ya mamlaka ya nani, kwa malengo gani ya kimkakati na kwa gharama ipi kwa taifa.

Hilo ndilo swali ambalo Bunge lina jukumu la kikatiba kujibu.

Asuman Kiyingi ni wakili mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Uganda, Mbunge wa zamani, na aliyekuwa Waziri wa Nchi wa Mambo ya Nje (Ushirikiano wa Kikanda).

Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

CHANZO:TRT Afrika