Maonesho ya Uturuki ya teknolojia ya anga maarufu TEKNOFEST yameanza Septemba 30. Maonesho hayo mwaka huu yanafanyika katika mkoa wa Sanliurfa uliopo kusini mashariki mwa nchi.
TEKNOFEST inaleta pamoja watu wenye shauku ya kubobea katika teknolojia na vijana wabunifu, pamoja na maelfu ya wageni wanaotembelea mabanda, na fainali za mashindano ya teknolojiga katika vipengele 14 kwa siku tano.
Teknofest ya mwaka huu itakamilika Oktoba 4.
Kama ilivyo kawaida, kutakuwa na maonesho ya anga na sekta ya ulinzi, pamoja na maonesho ya ndege za kivita za SoloTurk na Stars ya Uturuki.
Pia kutakuwa na maonesho ya ndege za Uturuki za Atak, Hurkus na Anka, pamoja na Bayraktar TB2, TB3 na droni za Akinci.
ZILIZOPENDEKEZWA
CHANZO:TRT World





















