Kituo maalumu cha habari kwa ajili ya mkutano wa NATO kimezinduliwa jijini Ankara.
Kituo hicho cha kisasa, kina vyumba vya 40 vya uhariri na vingine zaidi ya 100 vya kurushia matangazo ya moja kwa moja, kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.
Kurugenzi hiyo, imesisitiza kuwa, kituo hicho kimewekwa mahsusi kwa ajili ya kufanikisha mawasiliano wakati wote wa mkutano.
ZILIZOPENDEKEZWA
Jumla ya wafanyakazi 850 wanatarajiwa kuwepo ndani ya kituo hicho.
Wakati huo huo, chombo cha utangazaji cha wa TRT, kinatarajia kurusha matangazo ya mkutano huo moja kwa moja, kikitumia kamera 96 na magari ya matangazo 18 yatakayokuwa sehemu 26 tofauti.
CHANZO:AA



















