| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Lilikuwa ni jambo la kifahari kuandaa mkutano wa NATO jijini Ankara, asema Erdogan
"Tunaendelea kupokea jumbe na simu shukrani," anasema Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki.
Lilikuwa ni jambo la kifahari kuandaa mkutano wa NATO jijini Ankara, asema Erdogan
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa anaendelea kujisikia fahari na fuhara baada ya nchi yake kuandaa mkutano wa NATO, uliofanyika jijini

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa anaendelea kujisikia fahari na fuhara baada ya nchi yake kuandaa mkutano wa NATO, uliofanyika jijini Ankara.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari jijini Istanbul siku ya Ijumaa, Erdogan alisema kuwa anaendelea kupokea jumbe na simu za pongezi baada ya mkutano huo.

"Tunaendelea kupokea jumbe na simu za kutukushuru kutokana na ukarimu wetu. Viongozi wote, akiwemo Rais Donald Trump, walipata hisia tofauti na walituonesha hilo kabla na baada ya hafla," alisema Erdogan.

"Hata wale waliofika na wake zao walionesha furaha yao wa maonesho ya mavazi pamoja na mke wangu," aliongeza.

Wakati huo huo, Rais Erdogan alionesha furaha yake ya kuadhimisha miaka sita toka kufunguliwa kwa msikiti wa Ayasofya.

"Sifa ziende kwa Mungu kwa hatua hii. Tunajisikia furaha sana," alisema.

"Pia, tumepata heshima ya kuhifadhi msikiti huo kwa Waislamu."

Kulingana na Erdogan, ufunguzi wa eneo hilo, unatoa fursa kwa watu wote, wa dini mbalimbali, akiongeza kuwa ni jambo la furaha kwetu. Muonekano wa kihandisi wa msikiti huo ni jambo la kushangaza sana."

Katika mazungumzo yake ya simu na Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez kufuatia ushindi wa taifa hilo kwenye michuano ya Kombe la Dunia, Erdogan alisisitiza kuwa ni jambo la kawaida kwa Sanchez kuwa na furaha.

“Mungu akibariki, siku moja na sisi tutapata ushindi. Japo tulianza vizuro, mwisho haukuwa mzuri. Kuna michuano ya Ulaya katika siku zijazo, hiyo itakuwa fursa kwetu. Tutafurahi sana tukipata mafanikio," alieleza.

CHANZO:AA