| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Pep Guardiola aipongeza Arsenal kwa ushinidi wa EPL
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema Arsenal wanastahiki kuwa washindi.
Pep Guardiola aipongeza Arsenal kwa ushinidi wa EPL
Guardiola huenda ikawa ni msimu wake wa mwisho na timu ya Man City na nafasi yake kuchukuliwa na meneja wa zamani wa Chelsea, Enzo Maresca. / / Reuters

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameipongeza Arsenal F.C. na kocha wake Mikel Arteta baada ya klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL).

Matumaini ya Manchester City ya kupigania ubingwa yalimalizika baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Bournemouth, matokeo yaliyowafanya Arsenal kutangazwa mabingwa wa ligi hiyo huku ikiwa imebakisha mechi moja ya kumaliza msimu.

Mara ya mwisho Arsenal kushinda ubingwa huo ilikuwa chini ya kocha Arsene Wenger zaidi ya miaka 20 iliopita.

Aidha, ripoti kadhaa zinaeleza kuwa Guardiola huenda ikawa ni msimu wake wa mwisho na timu ya City na nafasi yake kuchukuliwa na meneja wa zamani wa Chelsea, Enzo Maresca.

CHANZO:TRT Afrika