Lengo halisi la Marekani na Israel kuzishambulia Iran ni lipi?
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Lengo halisi la Marekani na Israel kuzishambulia Iran ni lipi?Rais wa Marekani, Donald Trump, alieleza wazi kwamba hatua ya kuishambulia Iran ililenga kuizuia nchi hiyo kutengeneza silaha za nyuklia, pamoja na kushinikiza mabadiliko ya utawala.
Rais Donald Trump, anakabiliwa na shinikizo na baadhi ya wafuasi wake, wanaodai vita dhidi ya Iran ni kwa maslahi ya Israel na sio Marekani. / / Reuters

Mwanzoni mwa mgogoro huu, Rais wa Marekani, Donald Trump, alieleza wazi kwamba hatua ya kuishambulia Iran ililenga kuizuia nchi hiyo kutengeneza silaha za nyuklia, pamoja na kushinikiza mabadiliko ya utawala.

Vile vile, Marekani ilionyesha kuwa operesheni hiyo ingekuwa ya muda mfupi na yenye matokeo ya moja kwa moja.

Hata hivyo, hali imekuwa tofauti. Kufikia sasa, mgogoro huo umeingia katika wiki ya tano bila dalili yoyote ya kufanikiwa kubadilisha utawala wa Iran.

Hata baada ya kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, mfumo wa kisiasa haukusambaratika kama ilivyotarajiwa.

Kwa upande wake, Iran ilijibu kwa mashambulizi yaliyolenga Israel, kambi za kijeshi na mali za Marekani zilizoko katika nchi za Ghuba, na baadhi ya miundombinu ya kimkakati ya nchi hizo, pamoja na kufunga kwa Mlango wa Bahari wa Hormuz, ambayo ni njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani.

Kadiri mgogoro unavyoendelea, mwelekeo wa kauli za Marekani unaanza kubadilika.

Rais Trump ameanza kuzungumzia wazi nia ya kudhibiti rasilimali za mafuta za Iran, akisema: “Kwa ukweli kabisa, jambo ninalolipenda zaidi ni kuchukua mafuta ya Iran.”

Aidha, alilinganisha mkakati huo na Venezuela, akibainisha kuwa Marekani inalenga kudhibiti sekta ya mafuta kwa muda usiojulikana.

Pia alizungumzia uwezekano wa kuchukua maeneo ya kimkakati kama Kisiwa cha Kharg, akisema: “Huenda tukachukua Kisiwa cha Kharg, au tusichukue. Tuna chaguo nyingi,” na kuongeza kuwa hatua hiyo “ingemaanisha pia tungehitaji kubaki huko kwa muda.”

Akizungumzia uwezo wa Iran kujilinda katika eneo hilo, alisema: “Sidhani kama wana ulinzi wowote. Tunaweza kukichukua kwa urahisi sana.”

Pamoja na mvutano huo, Trump alidai kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yanaendelea, akisema: “Makubaliano yanaweza kufikiwa kwa haraka sana.”

Wakati huohuo, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amekuwa akisisitiza hadharani kuwa anashiriki katika kuunda upya ramani ya kisiasa ya Mashariki ya Kati. Katika moja ya kauli zake za wazi zaidi, alisema: “Tunabadilisha sura ya Mashariki ya Kati.”

Mabadiliko haya ya kauli na mikakati yanaibua swali muhimu: Je, hoja ya kuzuia silaha za nyuklia na kuleta mabadiliko ya utawala ilikuwa sababu halisi ya mgogoro huu, au ilikuwa ni pazia la kuficha malengo mapana zaidi, hasa udhibiti wa mafuta na ushawishi wa kikanda?

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Tumeshambulia kambi ya jeshi la Marekani nchini Kuwait: Vikosi vya Iran (IRGC)
Waislamu waswali swala ya Eid al-Adha katika Msikiti wa Al-Aqsa
Takriban Waislamu milioni 2 wanatarajiwa kutekeleza ibada ya Hajj huku mahujaji wakielekea Mina
Israel inahofia kuwa Trump atafuata makubaliano yenye mipaka ya Iran, na kuacha mpango wa nyuklia
'Wamepata vidonda mwilini' — wanaharakati wasimulia mateso waliyopitia walipotekwa na Israel
Mojtaba Khamenei amesema madini ya urani ya Iran yatabaki nchini humo
Marco Rubio: Tutahakikisha Ebola haifiki Marekani
Wanaharakati wa msafara wa Flotilla walioshambuliwa na Israel wapelekwa Uturuki
Trump na Netanyahu watofautiana kwa njia ya simu kuhusu kuishambulia Iran — Ripoti
Marekani na Israel zilipanga kumuweka madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo Ahmadinejad
Urusi na China zaimarisha ushirikiano kwa kusaini mikataba 20 ikiwemo ya uchumi, nishati na biashara
Mahakama ya ICC yatoa hati ya kukamatwa kwa Waziri wa Fedha wa Israel
Iran yatangaza bodi mpya ya kusimamia Mlango Bahari wa Hormuz
Marekani na Nigeria zafanya mashambulizi ya pamoja dhidi ya magaidi
Mahakama ya ICC imeripotiwa kutoa hati za siri za kukamatwa kwa maafisa watano wa Israel
Mkutano wa Trump-Xi: Mambo makuu yanayotokana na saa 9 ya mazungumzo ya makubwa nchini China
Israel, Lebanon wakubali kuongeza muda wa usitishaji mapigano kwa siku 45: Marekani
FBI yatoa zawadi ya Dola 200,000 kumsaka afisa wa Zamani wa Marekani anayetuhumiwa kujiunga na Iran
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz azomewa baada ya kuzinadi sera za serikali
Droni za Ukraine zaua 4 Urusi