| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Hakan Fidan wa Uturuki aongoza juhudi za kusitisha vita vya Mashiriki ya Kati
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan alijadili mwelekeo wa mzozo na juhudi za kusitisha mapigano katika mazungumzo na wenzake kutoka China, Syria, Qatar na Uzbekistan.
Hakan Fidan wa Uturuki aongoza juhudi za kusitisha vita vya Mashiriki ya Kati
Majadiliano hayo yalilenga "mwelekeo wa vita katika eneo hilo" na mipango inayolenga "kumaliza uhasama" katika vita. / Reuters / Reuters
tokea masaa 21

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, alizungumza kwa njia ya simu na wenzake kutoka China, Syria, Qatar na Uzbekistan kujadili mwenendo wa vita vinavyoendelea katika eneo hilo na juhudi za kuvimaliza, vyanzo vya kidiplomasia vilisema.

Kwa mujibu wa vyanzo vya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, Fidan alizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad Hassan al Shaibani, Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uzbekistan Bakhtiyor Saidov.

Majadiliano yalilenga “mwelekeo wa vita katika eneo hilo” na juhudi zinazoendelea za “kusitisha mapigano” katika vita hivyo, vilivyoanza Februari 28 wakati Marekani na Israel zilipoanzisha shambulio la pamoja dhidi ya Iran.

Fidan pia alizungumza kwa simu na mwenzake wa China Wang Yi na kujadili hali ya hivi karibuni katika eneo hilo, kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia vya Uturuki.

Katika mazungumzo hayo ya simu, mawaziri hao wawili walisisitiza kuwa vita vinavyoendelea katika Mashariki ya Kati lazima vikomeshwe haraka iwezekanavyo na walijadili juhudi za kufanikisha hilo.

Waziri hao walibainisha kuwa uendeshaji usiokatizwa wa njia za usafirishaji, usambazaji wa nishati, na minyororo ya ugavi ni muhimu sana.

Pande zote mbili pia zilijadili ajenda za mataifa mawili, hasa mahusiano ya kiuchumi na biashara, pamoja na uwekezaji wa pamoja.

Iran imelipiza kisasi kwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora yaliyolenga Israel, pamoja na Jordan, Iraq na vituo vya kijeshi vya Marekani zilizopo nchi za Ghuba, na kusababisha vifo na uharibifu wa miundombinu huku ikivuruga masoko ya dunia na usafiri wa anga.

Fidan amekuwa akifanya juhudi nyingi za kidiplomasia kumaliza vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati. Amezungumza mara kadhaa kwa njia ya simu na wenzake kutoka eneo hilo, wakiwemo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, pamoja na maafisa wa Marekani na Umoja wa Ulaya.

CHANZO:AA