| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Zaidi ya watu 30 wahofiwa kufa maji Uganda
Watu hao wanadaiwa kuwa waliwakuwa wakitoka kuvuna mkaa ndani ya msitu wa Bugoma kabla ya kupata ajali hiyo ndani ya Ziwa Nguse nchini Uganda.
Zaidi ya watu 30 wahofiwa kufa maji Uganda
Kulingana na Msemaji wa Polisi wa eneo la Albertine, Julius Hakiiza, hadi kufikia sasa, mwili mmoja umeopolewa katika eneo hilo./Picha:Wengine / Others

Zaidi ya watu 30 wanahofiwa kufa maji nchini Uganda baada ya boti waliyokuwa wakisafiria, kuzama ndani ya Ziwa Nguse , usiku wa Jumanne.

Watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakitoka kuvuna mkaa ndani ya msitu wa Bugoma kabla ya kupata ajali hiyo.

Tukio hilo linaripotiwa kutokea katika kijiji cha Kyaleni katika Manispaa ya Pachwa.

Kulingana na Msemaji wa Polisi wa eneo la Albertine, Julius Hakiiza, hadi kufikia sasa, mwili mmoja umeopolewa katika eneo hilo.

Uchunguzi wa awali, unaonesha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na chombo hicho kujaa kupita uwezo wake wa kawaida.

CHANZO:TRT Afrika Swahili