Makamu wa Rais wa Tanzania, Balozi Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kuanzia Septemba 4, 2026, chini ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika barua ya Agosti 25, 2026 iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Nchimbi amesema amemwandikia Rais Samia kumjulisha kuwa ameamua pia kustaafu siasa na utumishi wa umma.
Balozi Emmanuel Nchimbi alichaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Dkt. Emmanuel John Nchimbi alizaliwa miaka 54 iliyopita. Ana shahada ya uzamivu katika masuala ya uongozi.
Amekuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya wilaya, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) na mjumbe wa halmashauri kuu. Pia alipata kuwa mbunge wa jimbo la Songea Mjini.
Kabla ya kuwa Balozi, alihudumu katika nyadhifa za naibu waziri wa habari, pia alikuwa naibu katika wizara ya kazi na vijana pamoja na ulinzi. Amewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri na katika taifa la Brazil.
Amewahi pia kuwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baba yake John Alfonso Nchimbi alikuwa afisa wa jeshi la polisi mwandamizi na alifariki dunia 2022.




















