| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Iran yasema mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon ni ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian aonya kuwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon yataathiri makubaliano ya kusitisha mapigano.
Iran yasema mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon ni ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian aikosoa Israel kwa kuishambulia Lebanon. / / Reuters
tokea masaa 3

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kupitia ukurasa wake wa X kuwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon ni ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano, akionya kuwa hali hiyo inaweza kuhatarisha juhudi za kidiplomasia zinazoendelea katika eneo hilo.

Rais huyo alisema, “Uchokozi unaorudiwa na dola ya Kisayuni dhidi ya Lebanon ni ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano. Kuendelea kwa vitendo hivi kutafanya mazungumzo kukosa maana. Iran haitowatelekeza ndugu zake wa Lebanon.”

Aliongeza kuwa ni ishara hatari ya udanganyifu na ukosefu wa dhamira katika kuheshimu makubaliano yanayoweza kufikiwa.

Kauli hiyo imekuja wakati mashambulizi mapya ya Israel ndani ya Lebanon yakiripotiwa kusababisha vifo vya watu wengi, huku mvutano ukiendelea kuongezeka licha ya kuwepo kwa makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano.

CHANZO:TRT Afrika