Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwezekano wa mvua kubwa zitakazoweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya mikoa ya ukanda wa Pwani, ikiwemo Dar es Salaam.
TMA imeeleza kuwa uwezekano wa mvua hizo pamoja na athari zake uko katika kiwango cha kati, huku wananchi wakitakiwa kuchukua tahadhari zote muhimu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uwezekano wa mvua pamoja na athari zake umeainishwa kuwa wa kiwango cha kati, lakini wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari zote muhimu.
“Kuanzia leo hadi Ijumaa, mvua zinatarajiwa kunyesha katika maeneo tajwa. Uwezekano na athari zake zipo katika kiwango cha kati,” imeeleza taarifa ya TMA.
TMA imetahadharisha kuwa mvua hizo zinaweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo na kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi.












