Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, amempandisha cheo mwanaye anayehudumu ndani ya Jeshi la taifa la nchi hiyo (ZNA).
Sean Mnangagwa, ambaye ni sehemu ya kikosi cha ulinzi wa rais, amepandishwa cheo kutoka kuwa Meja hadi ngazi ya Luteni Kanali, mabadiliko ambayo yamezua gumzo kwa sasa nchini humo.
Akiwa na umri wa miaka 39, amekuwa ni sehemu ya ulinzi wa rais tangu alipojiunga na jeshi mwaka 2010.
Wakati huo, baba yake, Emmerson Mnangagwa, alikuwa akihudumu kama Waziri wa Ulinzi wa Zimbabwe, chini ya utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe.
Sean Mnangagwa alipata mafunzo yake ya kijeshi katika nchi mbalimbali, zikiwemo Zimbabwe, China, Urusi na Msumbiji.
CHANZO:TRT Afrika Swahili
















