Zaidi ya watu wa 100,000 wameshiriki katika maandamano ya nchi nzima huko Ufaransa siku ya Jumanne, baada ya vyama vya wafanyakazi kuitisha mgomo wa nchi nzima.
Kupitia mgomo huo, vyama hivyo vinadai nyongeza za mishahara.
Kati ya washiriki wa maandamano hayo, ni pamoja na wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu, ambao walijiunga na waandamanaji kutoka sekta binafsi, wakiishinikiza serikali ya nchi hiyo kushughulikia suala la kupanda kwa gharama za maisha.
Ufaransa imekumbwa na maandamano kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja, wakati ambapo serikali ya nchi hiyo ipo katika hatua za kupitisha mpango wa kubana matumizi, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mwakani.
Katika mitaa mbalimbali ya jiji la Paris, waandamanaji walibeba ngoma zao, huku wengine wakipiga muziki kwa sauti ya juu, kuonesha hisia zao kwa kupanda kwa gharama za maisha nchini humo.





















