| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Wafanyakazi wa shirika la ndege la Lufthansa kufanya mgomo
Kufuatia hali hiyo, abiria shirika hilo walishauriwa kuangalia ratiba za ndege zao kabla ya kupanga safari zao.
Wafanyakazi wa shirika la ndege la Lufthansa kufanya mgomo
Ndege za Shirika la Ndege la Lufthansa./Picha:@airplusnews/
tokea masaa 4

Wafanyakazi wa shirika la ndege la Lufthansa wamepanga kufanya mgomo wa siku moja siku ya Ijumaa na kutishia kuzorotesha huduma za usafiri katika majiji ya Frankfurt na Munich.

Mgomo huo unakuja wakati ambapo umoja wa wafanyakazi hao, ukilituhumu shirika la Lufthansa kwa kushindwa kutimiza ahadi ya kuboresha mazingira yao kazi ya wafanyakazi wao.

Kulingana na umoja huo (UFO), mazungumzo ya uboreshaji wa mazingira ya wafanyakazi hao yameshindwa kufanyika, na hivyo wao kutokuwa na budi bali kuendelea na mgomo.

Kufuatia hali hiyo, abiria shirika hilo walishauriwa kuangalia ratiba za ndege zao kabla ya kupanga safari zao.

CHANZO:AA