| Swahili
Maoni
AFRIKA
3 dk kusoma
Namna vita vya Iran vinavyoathiri uchumi wa Afrika na siasa.
Afrika inaagiza zaidi mafuta yaliyosafishwa, jambo linalofanya itatizike kwa kutokana na yanayoendelea duniani. Kupanda kwa bei za mafuta kutokana na vita vya Iran tayari kunasababisha mfumuko wa bei, na kupanda kwa gharama za maisha.
Namna vita vya Iran vinavyoathiri uchumi wa Afrika na siasa.
PICHA YA MAKTABA: Bei za Mafuta zimepanda barani Aftika huku vita vya Iran vikiathiri usambazaji / Reuters
tokea masaa 6

Vita vya Iran vinaweza kuwa umbali wa maelfu ya kilomita kutoka Afrika, lakini athari zake tayari zinarindima kote barani. Kutoka kwa bei za juu za mafuta Afrika Mashariki hadi kwa matatizo ya fedha kusini, mzozo huu umedhihirisha udhaifu wa uchumi wa nchi za Afrika.

Changamoto za kiuchumi

Athari ya moja kwa moja imeonekana kwenye masoko ya nishati. Afrika inaagiza zaidi mafuta yaliyosafishwa, jambo linalofanya itatizike kwa kutokana na yanayoendelea duniani. Kupanda kwa bei za mafuta kutokana na vita vya Iran tayari kunasababisha mfumuko wa bei, na kupanda kwa gharama za maisha.

Kutatizwa kwa njia za meli, hasa kupitia Mlango Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya kupitisha mafuta ya dunia, kumesababisha bei za mafuta kupanda sana. Nchi kama Kenya, Uganda, na Somalia zinakabiliwa na uhaba wa mafuta na kupanda kwa gharama, huku baadhi ya serikali zikitoa wito kwa raia kuepuka kununua bidhaa kutokana na hofu.

Hata nchi ambazo zinazalisha mafuta hazijaepuka msumeno huu. Kwa mfano, Nigeria, inaendelea kuagiza sehemu kubwa ya mafuta yanayosafishwa, kufanya iwe vigumu kujikinga na bei kubwa za mafuta duniani. Kote barani Afrika, watunga sera wanaonya kuwa kuongezeka kwa bei ya nishati kunaweza kukadumaza uchumi ambayo tayari unasuasua na kulazimisha benki kuu kutafakari kuhusu sera zake za fedha.

Kilimo pia kimetatizika. Bei za mbole zimefungamana na masoko ya nishati zinapanda, kutishia uzalishaji wa chakula na upatikanaji wake. Taarifa kutoka kwa maafisa wa Afrika zimeonya kuwa kuongezeka huku kunaweza kusababisha kupanda kwa bei za vyakula na kufanya hali kuwa mbaya zaidi.

Kinachobainika siyo athari za wazi pekee, lakini kuendelea kwake, zikidhihirisha mifumo midogo ya kupanua wigo wa upatikanaji wa chakula, nishati, na ushirikiano wa kibiashara.

Kutatizwa kwa biashara.

Vita vya Iran vimezidisha hali ya taharuki katika shoroba za baharini, hasa katika Bahari ya Shamu na Ghuba. Njia hizi ni muhimu kwa biashara barani Afrika, zinazounganisha bara na masoko ya dunia ya mafuta, mbolea na bidhaa zinazotumika kila siku.

Kutatizika huku pia kunaleta fursa. Huku mienendo ya usafiri wa baharini ikisuwasuwa, njia mbadala kama vile ya Cape of Good Hope inatumia zaidi. Hili tayari limetoa nafasi kwa meli kuongeza mafuta katika baadhi ya mataifa ya kusini mwa Afrika.

Hili linadhihirisha umuhimu wa kimkakati wa bandari za Afrika na shoroba zake. Fursa hizi huenda zikawaponyoka pia.

Muda wa kutafakari.

Vita vya Iran siyo tu tatizo la kutoka nje. Ni jaribio kwa uthabiti wa uchumi wa Afrika, mifumo ya biashara, na utashi wa kisiasa. Bara hili halikuanzisha mzozo huu, lakini kwa mara nyingine linajikuta likiathirika kwa kupanda kwa bei, kutatiza maisha ya watu,na kuwa na sera tatanishi.

Mafunzo yako wazi. Kutegemea sana kuagiza mafuta, uwezo mdogo wa viwanda, na kutoshirikiana vyema kikanda kunazidisha hali kuwa mbaya zaidi. Bila kuchukua hatua madhuburi, hali hii itaendelea.

Lakini kipindi hiki pia kinatoa fursa. Uwekezaji katika nishati endelevu, ushirikiano thabiti kupitia biashara huru barani Afrika, na ustahmilivu katika kukabiliana na mifumo ya usambazaji huenda kukapunguza matatizo katika siku zijazo.

Uratibu wa diplomasia unaweza kuruhusu mataifa ya Afrika kujadiliana yakiwa na nguvu katika mazingira ambayo dunia haizungumzi kwa kauli moja.

Swali siyo kama Afrika imeathirika. Swali haswa ni kama kipindi hiki, bara litakabiliana na hali hii kwa nia tofauti.

Mwandishi, Hafsa Abdiwahab Sheikh, ni mwandishi habari huru na mtafiti anayeangazia siasa za Afrika Mashariki.

CHANZO:TRT Afrika