| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Usafiri katika Mlango Bahari wa Hormuz umezidi kupungua katika kipindi cha wiki tano
Usafiri wa meli kupitia njia ya maji ya kimkakati unashuka kwa sababu ya mapigano mapya ya Marekani-Iran na mashambulizi dhidi ya meli yanayoongeza wasiwasi wa usalama katika Ghuba.
Usafiri katika Mlango Bahari wa Hormuz umezidi kupungua katika kipindi cha wiki tano
Meli zikipita katika Mlango wa Bahari wa Hormuz. / Reuters

Idadi ya meli zinazopita katika Mlango Bahari wa Hormuz imepungua katika kipindi cha wiki tano kufikia Jumapili, huku mashambulizi ya meli ya Marekani na Iran katika eneo la Mashariki ya Kati yakiendelea kuongeza hali ya wasiwasi.

Meli sita zimepita katika Mlango Bahari Jumapili, kwa mujibu wa taarifa zinazofuatilia safari za meli Kpler.

Miongoni mwa meli zilizopita Hormuz ni meli kubwa ya mafuta ghafi Humanity, inayobeba mapipa milioni 2 ya mafuta ya Iran, na meli ya Capetan Andreas, inayobeba takriban mapipa 500,000 ya bidhaa za mafuta ya Kuwait.

Meli tatu tupu, ziliingia eneo la Ghuba kubeba mafuta ghafi, huku meli nyingi zikizima mawasiliano yake wakati zikiingia Hormuz, taarifa imeonesha.

Hakuna meli ya gesi iliyoonekana ikiingia eneo la Hormuz mwishoni mwa juma, kwa mujibu wa taarifa za ufuatiliaji wa safari za meli.

Taarifa za Kpler pia zimeonesha kuwa ni meli moja pekee inayoendeshwa na shirika la mafuta la taifa la Abu Dhabi ambayo imetoka eneo la Hormuz kati ya Julai 10 na Julai 12. Meli hiyo inaekelea bandari ya Dahej nchini India.

Kamandi Kuu ya Marekani imesema vikosi vyake vimefanya mashambulizi mengine dhidi ya Iran Jumapili, vikilenga maeneo kadhaa.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Jumapili kwamba Mlango Bahari wa Hormuz unaendelea kuwa wazi kwa meli za biashara. Mwanzoni, Iran imesema imefunga eneo hilo, ikidai meli iliyopita bila idhini imeshambuliwa.

Vikosi vya Iran vimesema Jumatatu kwamba vikosi vyake vya majini vimezuia meli mbili katika Mlango Bahari wa Hormuz usiku wa kuamkia Jumatatu kwa kuzuia mifumo yao. Taarifa hiyo haikufafanua kuhusu meli hizo.