| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Mahakama ya Marekani yaamuru 'kufurushwa' kwa raia wa Haiti na Syria
Uamuzi wa mahakama hiyo iliyojaa wahafidhina, huenda ukaathiri wanufaika takribani milioni moja wa mradi wa hifadhi wa TPS nchini Marekani.
Mahakama ya Marekani yaamuru 'kufurushwa' kwa raia wa Haiti na Syria
Rais Donald Trump wa Marekani./Picha:Reuters / Reuters

Mahakama Kuu nchini Marekani, imeamuru kutumuliwa kwa raia 350,000 wa Haiti na wengine 6,000 kutoka Syria, ambao kwa sasa wanaishi nchini humo.

Uamuzi wa mahakama hiyo iliyojaa wahafidhina, huenda ukaathiri wanufaika takribani milioni moja wa mradi wa hifadhi wa TPS nchini Marekani.

Kupitia hukumu yake iliyoungwa na majaji wengine watano wenye mrengo kihafidhina, Jaji Samuel Alito, alibainisha kuwa uamuzi wa Idara ya Usalama wa Ndani ya Marekani, haukupaswa kufanyiwa uhakiki wa ziada.

Hata hivyo, Jaji Alito alisisitiza kuwa hukumu haihusiani na uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuwanyang’anya raia wa Haiti na Syria hadhi ya TPS.

Kwa upande wao, wanasheria wa raia hao wanaoondolewa nchini Marekani, wamepinga hukumu hiyo, wakidi kuwa mazingira nchini mwao si salama kwa wao kurudi.

CHANZO:AFP