| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Nigeria yaharibu silaha haramu 2,819 katika kukabiliana na utovu wa usalama
Shirika la kudhibiti silaha nchini Nigeria siku ya Alhamisi lilisema kuwa limeharibu na kuvunja silaha haramu 2,819, katika juhudi za kukabiliana na ukosefu wa usalama.
Nigeria yaharibu silaha haramu 2,819 katika kukabiliana na utovu wa usalama
Uharibifu wa silaha unafanyika wakati Nigeria ikikabiliana na ujambazi, utekaji nyara, na ugaidi

Shirika la kudhibiti silaha nchini Nigeria lilisema siku ya Alhamisi kuwa limeharibu na kuvunja silaha haramu 2,819, katika juhudi za kukabiliana na ukosefu wa usalama na kuenea kwa silaha haramu.

Mkuu wa shirika hilo Johnson Kokumo anasema silaha hizo ziliharibiwa hadharani kiasi cha kutoweza kutumika tena kwa lengo la kuzuia kurejea mikononi mwa watu wasio na nia njema.

Uharibifu huo unafanyika wakati Nigeria ikikabiliana na ujambazi, utekaji nyara, ugaidi na vurugu katika jamii, ambayo mamlaka zinasema yamechangiwa na uwepo wa silaha haramu.

Maafisa wanasema silaha zaidi ya 21,000 zimepatikana tangu kuanzishwa kwa shirika hilo mwaka 2021 na zaidi ya 19,000 zimeharibiwa kabisa na haziwezi kutumika tena.

CHANZO:TRT Afrika Swahili