| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Trump apanga kuwahamisha raia wa Iran kutoka Marekani hadi Jamhuri ya Afrika ya Kati
Idara ya Rais Trump yapanga kuwafukuza baadhi ya raia wa Iran pamoja na wahamiaji wengine kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa mujibu wa mawakili wawili na afisa mmoja aliyefahamishwa kuhusu suala hilo, ambao walizungumza na Reuters.
Trump apanga kuwahamisha raia wa Iran kutoka Marekani hadi Jamhuri ya Afrika ya Kati
Wairan na Wasyria ni miongoni watakaohmishwa kutoka Marekani hadi Jamhuri ya Afrika ya Kati. / / AP

Miongoni mwa raia wa Iran wanaopangwa kuhamishwa ni wanawake wawili, kwa mujibu wa wakili wao, Emily Trostle.

Wanawake hao wawili waliomba hifadhi nchini Marekani na walikuwa wamepewa ulinzi wa kisheria unaozuia kufukuzwa kurejeshwa Iran, alisema Trostle.

Afisa huyo aliyepewa taarifa kuhusu mpango huo aliiambia Shirika la Habari la Reuters kwamba ndege ya kwanza kuelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati chini ya makubaliano hayo ilitarajiwa kubeba takriban watu 20, wakiwemo pia raia wa Syria na Afghanistan. Kulingana na mawakili hao wawili, ndege hiyo inaweza kuondoka Alhamisi.

Mashambulizi dhidi ya Iran

Utawala wa Trump umetumia makubaliano ya kuwapeleka wahamiaji katika nchi zinazoendelea ili kuwafukuza watu ambao hauwezi kisheria kuwarudisha katika nchi zao za asili. Serikali ya Marekani imetetea makubaliano hayo ikisema ni halali kisheria.

Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi ya pamoja dhidi ya Iran mwishoni mwa Februari, jambo lililoanzisha vita ambavyo sasa vimefikia takriban miezi mitatu.

Rais wa Marekani Donald Trump aliwaambia waandishi wa habari mwezi Aprili kwamba aliamini wananchi wa Iran wanapaswa kuasi dhidi ya serikali yao ikiwa usitishaji wa mapigano utatangazwa, lakini alikiri kuwa kufanya hivyo kungekuwa hatari sana kwao.

Kwa mujibu wa afisa huyo, watu watakaofukuzwa watahifadhiwa katika vyumba vya makazi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, na hawatarajiwi kurejeshwa mara moja katika nchi zao za asili. Afisa huyo aliongeza kuwa mamia ya wahamiaji wanaweza hatimaye kupelekwa huko chini ya makubaliano hayo.

IOM yasema haijahusika katika makubaliano ya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mpango wa kuwafukuza Wairani hao uliripotiwa mapema Alhamisi na gazeti la The New York Times.

Wiki iliyopita, Wizara ya Mambo ya Ndani (DHS) ilisema kwamba watu wote watakaofukuzwa watapatiwa haki kamili za kisheria.

Msemaji wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) alisema shirika hilo “litatoa msaada wa kibinadamu baada ya kuwasili” kwa wahamiaji watakaopelekwa Bangui, kwa ombi la serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Msemaji huyo alisisitiza kuwa IOM haikushiriki katika zoezi la kuwahamisha wahamiaji hao, na kwamba msaada wake utatolewa “kwa hiari kabisa na kwa kuzingatia viwango vinavyotumika kimataifa.”

Mwaka huu, Marekani imetoa Dola milioni 85 za Marekani kwa IOM kwa ajili ya shughuli zake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, nchi yenye idadi ya watu takriban milioni 5.5.

CHANZO:Reuters