Watu wengi kutoka mataifa 36 hawaipendi Israel na hawana imani na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kulingana na utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Utafiti la Pew.
Utafiti huo, uliotolewa siku ya Alhamisi na kufanywa kati ya Februari 8 - Mei 13, 2026, umebaini kuwa wastani wa dunia wa asilimia 67 ya watu wazima hawaipendi Israel, huku asilimia 25 ikiegemea upande wa Israel.
Maoni haya ya kutopendwa yalikusanywa zaidi katika mataifa yenye Waislamu wengi, ikiwemo Bangladesh, Indonesia, Malaysia, Pakistan, Uturuki, eneo linalokaliwa la Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki.
Wengi ya wale waliohojiwa katika mataifa yao wanasema wana imani ndogo au hawana imani kabisa kuwa Netanyahu atafanya jambo sahihi katika masuala ya ulimwengu, utafiti ulisema.
Kenya na Ufilipino ndiyo mataifa pekee ambayo zaidi ya nusu ya raia wake wameeleza kuwa na imani na waziri mkuu wa Israel, umeongeza.
Kutoipenda Israel kuomeongezeka katika mataifa 13 kati ya 24 ambapo taarifa zilikuwepo tangu 2025, inasema Pew.





















