| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Jeshi la Sudan laangusha 'droni za adui' ambazo hazijatambuliwa jimbo la Kassala
Mifumo ya ulinzi ya anga ya jeshi la Sudan imeangusha droni kadhaa za wapiganaji ambazo zilikuwa zinashambulia maeneo ya kaskazini mwa Omdurman.
Jeshi la Sudan laangusha 'droni za adui' ambazo hazijatambuliwa jimbo la Kassala
Hali ya kawaida imeanza kurudi taratibu katika mji wa Khartoum huku juhudi za ujenzi upya zikiendelea. / AFP

Jeshi la Sudan limeangusha droni kadhaa mashariki mwa nchi, kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo siku ya Jumanne.

Droni hizo ziliangushwa na mifumo ya ulinzi wa anga eneo la Al-Fashaga la jimbo la Gedaref na Khashm al-Girba jimbo la Kassala, gazeti la the daily Sudan News limeripoti.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa droni hizo ni za “adui,” bila kutaja asili yake au kutoa taarifa kuhusu walioathirika au uharibifu.

Haya yanajiri siku tano baada ya jeshi la Sudan kuangusha droni ya wapiganaji RSF karibu na mji mkuu, Khartoum.

Mifumo ya ulinzi wa anga ya jeshi la Sudan imekuwa ikikabiliana na kuangusha droni kadhaa za wapiganaji ambazo zilijaribu kushambulia maeneo kaskazini mwa Omdurman, sehemu ambayo ina jeshi kubwa na karibu na mji wa Khartoum.

Mwezi Januari mwaka huu, Hamid Ali Abubakar, mshauri wa usalama wa kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, aliuawa pamoja na maafisa wengine katika shambulio la droni lililofanywa na jeshi la Sudan karibu na mji wa Zalingei.

Tangu Aprili 2023, ​​​​​​​Sudan imegubikwa na mapigano kati ya jeshi na RSF, vita ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaondoa mamilioni wengine katika makazi yao.

CHANZO:TRT Afrika and agencies