Serikali ya Iran imetangaza siku tatu za mapumziko, kupisha mazishi ya aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa taifa hilo, Ayatollah Ali Khamenei.
"Ibada ya mazishi kwa kiongozi wetu itafanyika Julai 4 na 5, huku mazishi yenyewe yakifanyika Julai 6, na siku hiyo itakuwa ni ya mapumziko katika jiji la Tehran," alisema Hassan Hassanzadeh, ambaye pia ni kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), anayehusika na sherehe mbalimbali.
Mapema Jumanne, chombo cha habari cha serikali ya Iran, kilitangaza kuwa Julai 4 na 5 kuwa siku za mapumziko kwa jiji la Tehran, huku nchi nzima ikiingia mapumzikoni Julai 6.
Jiji la Tehran linatarajia kushuhudia watu milioni 20 wakihudhuria mazishi hayo.
Ali Khamenei anatarajia kuzikwa Julai 9, katika mji wa kaskazinimashariki mwa mji wa Mashhad, mahali alipozaliwa kiongozi huyo.
Ibada hiyo ilipangwa kufanyika mwezi Machi, lakini ilisogezwa mbele kufuatia vita katika eneo la Mashariki ya Kati.





