| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Iran: Hatuna mazungumzo yoyote na Marekani
Iran imekuwa na udhibiti wa njia hiyo toka kuanza kwa vita vya Mashariki ya Kati, Februari 28.
Iran: Hatuna mazungumzo yoyote na Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Esmaeil Baqaei amesema kuwa taifa hilo halijafanya mazungumzo yoyote na Marekani kuhusu mustakabali wa Mlango Bahari

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Esmaeil Baqaei  amesema kuwa taifa hilo halijafanya mazungumzo yoyote na Marekani kuhusu mustakabali wa Mlango Bahari wa Hormuz.

"Hatuna mazungumzo yoyote na Marekani, isipokuwa tuna mazungumzo na Oman kuhusu Oman kwa ajili ya Mlango Bahari wa Hormuz,” alisema waziri huyo.

Iran imekuwa na udhibiti wa njia hiyo toka kuanza kwa vita vya Mashariki ya Kati, Februari 28, mwaka huu.

Wakati huo huo, Iran imesisitiza kuwa njia hiyo itaendelea kurahisisha usafirishwaji wa nishati mbalimbali, kwa kupata kibali kutoka Iran.

Akizungumzia mazungumzo na Oman, Baqaei alisema kuwa, yanaridhisha, yakiwa na lengo la kuzindua njia mpya ya kupitia.

"Ni matumaini yetu kuwa, wenzetu watakubaliana na mpango huu,” alieleza.

 

 

CHANZO:AFP
Soma zaidi
Ghalibaf: Hakuna nchi itakayoweza kuuza mafuta ikiwa Iran itazuiwa kuuza
Bingwa wa zamani wa ‘Pool Table’ Graeme Dott atupwa jela miaka saba kwa kuwanyanyasa watoto kingono
Iran yakana kuhusika na njama ya kulipua kituo cha anga cha Uingereza kinachotumiwa na Marekani
Trump akataa pendekezo la Iran la kufungua tena Mlango-bahari wa Hormuz
Iran yapendekeza makubaliano na Marekani kufungua  Mlango-bahari wa Hormuz ndani ya siku saba
Korea Kaskazini yasema itaendelea kuzalisha silaha za kinyuklia
Jeshi la Israel lalipua makazi ya mfungwa wa Kipalestina
Wanafunzi warejea mashuleni baada ya vita kumalizika Iran
Ujerumani yagomea wito wa Trump wa kujiondoa ICC
Je, China inaweza kubadilisha uhusiano wao na Iran kuwa wa kidplomasia kabla ya mkutano wa Xi-Trump?
Qatar yataka mfumo wa usalama kati ya nchi za Ghuba na Iran kufuatia mzozo unaoendelae
Trump kutolishambulia kundi la Wa-Houthi kwa sasa: Gazeti la NYT
Italia inapanga kupiga marufuku kufunika uso shuleni na kuweka kikomo kwa wanafunzi wa kigeni
Jeshi la Marekani linakadiria gharama ya vita dhidi ya Iran kuwa Dola bilioni 43.6
Trump atia saini mswada wa vikwazo dhidi ya Urusi: China na India zakabiliwa na uwezekano wa ushuru
Kaka wa Princes Diana ‘amshukia’ Mfalme Charles III kwa kufurahia kifo cha dada yake
Mtu mmoja afa kwa ugonjwa wa Malaria nchini Ujerumani
Trump: Iran imewasiliana moja kwa moja na Marekani, inataka kufikia makubaliano
Marekani yaingia mkataba wa kuvuna mafuta na dhahabu ya Venezuela
Pakistan yalaani “jaribio la shambulio la droni” karibu na Makkah