Tanzania: Panga Pangua ya Rais Samia
ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
Tanzania: Panga Pangua ya Rais SamiaLakini swali la baadhi kuondoka na kurudi, hilo linamaanisha nini hasa?
Rais anaimarisha safu yake wakati nchi ikijiandaa na uchaguzi wa serikali za mtaa unaotarajiwa kufanyika mwakani. Picha: Getty / Others

Kama umekuwa makini kufuatilia mambo mwaka huu, bila shaka utakuwa umeona mabadiliko mengi yaliyofanywa na rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika safu yake ya uongozi – hii ni kuanzia mabadiliko ya baraza la mawaziri hadi wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali.

Mabadiliko haya yamekuwa yakifanyika mara kwa mara na ndani ya mufa mfupi katika kipindi cha mwaka mmoja. Ingawa katiba ya Tanzania, inampa mamlaka kamili rais kuteua na kutengua, lakini kasi yake ya uteuaji na utenguaji ndiyo inayoibua mjadala mpana miongoni mwa wananchi.

Wataalamu wa masuala ya uongozi wanaitetea hatua hiyo ya rais, na kusema kuwa, rais ni kama kocha wa mpira, anauwezo wa kubadilisha safu yake wakati wowote anapohisi kufanya hivyo kutaleta ufanisi wa utendaji wa serikali yake.

Hata hivyo, maswali mingi pia yanaibuka pale mtu mmoja anapotenguliwa zaidi ya mara moja, na baadae kuteuliwa tena katika nafasi hiyo hiyo.

Mathalan, mwezi Septemba mhandisi Peter Ulanga yalimkuta ya kutenguliwa na baada ya siku mbili kuteuliwa tena katika nafasi hiyo hiyo. Watu walimaka, lakini rais alijitetea kwa kusema kulikuwa na kosa la utafiti duni uliofanywa na timu yake ya washauri.

Mwenendo huu, unaonekana kuanza kujenga khofu miongoni mwa watumishi wa umma. Rais Samia mwenyewe anakiri katika hilo, lakini anagongea msumari kwa kuwataka viongozi wazembe kukaa chonjo.

Lakini pia, pangua pangua hii inaweza kuwa ya kimkakati. Rais anaimarisha safu yake wakati nchi ikijiandaa na uchaguzi wa serikali za mtaa unaotarajiwa kufanyika mwakani. Tupe maoni yako kuhusu haya yanayojiri.

➤ Fuatilia TRT Afrika Swahili kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Israel yathibitisha mwanajeshi wake kuharibu sanamu ya Yesu kwa kutumia nyundo
Iran ‘yanyonga’ Waisrael wawili kwa kuhusika na mtandao wa kijasusi wa Israel
Mkuu wa Mji wa Tel Aviv afichua zaidi ya nyumba 1,000 haziwezi kukaliwa kutokana na vita vya Iran
Trump asema Marekani itatwaa urani ya Iran nyumbani kwa kutumia 'mashine kubwa za uchimbaji'
Makombora ya Urusi yashambulia Ukraine na kuua watu 16
Iran yapendekeza miaka 5 ya kusitisha urutubishaji wa Uranium huku Marekani ikishinikiza miaka 20
Meli ya China iliowekewa vikwazo na Marekani yapita Mlango Bahari wa Hormuz
Zaidi ya theluthi moja ya miundombinu ya nishati Mashariki ya Kati imeathiriwa na vita vya Iran
Gazeti la Uingereza la The Daily Telegraph lafuta habari isiyo sahihi kuhusu Erdogan
Trump afikiria kuishambulia upya Iran baada ya mazungumzo ya amani ya Islamabad kushindikana-ripoti
Trump aagiza jeshi la Marekani kukamata meli yoyote inayolipa kuvuka mlango bahari wa Hormuz
Takriban watu 30 wamefariki katika mkanyagano kwenye ngome ya kihistoria ya Laferriere nchini Haiti
Hakuna makubaliano ya Marekani-Iran baada ya mazungumzo ya saa 21 nchini Pakistan, asema Vance
Marekani yakubali kuachilia mali ya Iran iliyozuiliwa ili kuendeleza mazungumzo ya Islamabad
Makamu wa Rais Vance awasili Pakistan kuanza mazungumzo muhimu ya Marekani na Iran
Korea Kaskazini, China zakutana, kukuza ushirikiano wa kimkakati
Rais Macron, Papa Leo wa 14 wajadili hali ya Mashariki ya Kati
Netanyahu asema Israel itaishambulia Hezbollah pale inapobidi
Kocha wa zamani wa Romania Mircea Lucescu afariki dunia
Bilionea Bill Gates kutoa ushahidi wake kuhusu faili za Jeffrey Epstein