| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
CCM na ACT-Wazalendo wamaliza mgogoro wa kisiasa Zanzibar
Hatua hii ya uwasilishwaji wa Tamko la Pamoja la Muafaka wa Kisiasa inaashiria kumalizika kwa mkwamo wa kisiasa.
CCM na ACT-Wazalendo wamaliza mgogoro wa kisiasa Zanzibar
Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar Julai 9, 2026. /@Ikulu_Tanzania / X

Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman wameshuhudia utiaji saini wa ajenda zilizokubaliwa na pande zote mbili kwa ajili ya kufanyiwa kazi baada ya Tamko la Pamoja la Muafaka wa Kisiasa baina ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo, katika viwanja vya Ikulu Zanzibar tarehe 09 Julai, 2026.

Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar Julai 9, 2026.

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, muundo wa serikali yake ni wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambapo chama tawala huunda serikali na chama cha upinzani kinachoshika nafasi ya pili katika Uchaguzi Mkuu, kwa kuchukua nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais pamoja na nafasi kadhaa za uwaziri.

Hata hivyo, tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, kumekuwa na msuguano kati ya CCM na ACT-Wazalendo, hivyo kuchelewesha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Hatua hii ya uwasilishwaji wa Tamko la Pamoja la Muafaka wa Kisiasa inaashirika kumalizika kwa mkwamo huo wa kisiasa.

CHANZO:TRT Afrika