| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Rais Faye wa Senegal aunda serikali mpya bila chama cha Sonko
Senegal inakabiliwa na hali ya sintofahamu ya kisiasa baada ya Rais Faye kutangaza baraza jipya la mawaziri ambalo halijajumuisha chama tawala cha PASTEF kinachoongozwa na mshirika wake wa zamani, Ousmane Sonko.
Rais Faye wa Senegal aunda serikali mpya bila chama cha Sonko
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye aliingia madarakani mnamo Aprili 2024. / / Other

Rias wa Senegal Rais Bassirou Diomaye Faye amemteua mwanauchumi Ahmadou Al Aminou Lo kuwa Waziri Mkuu mpya, akisema ana uzoefu unaohitajika kukabiliana na mgogoro wa deni la taifa.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa Faye mwezi Mei kumtimua Sonko katika nafasi ya uwaziri mkuu, jambo lililodhihirisha mpasuko mkubwa unaoendelea kati ya viongozi hao wawili ambao hapo awali waliongoza pamoja harakati za upinzani nchini humo.

Sonko alianzisha chama cha PASTEF mwaka 2014 na alichangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa Faye hadi kuwa Rais. Baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2024, Faye alimchagua Sonko kuwa Waziri Mkuu, lakini baadaye tofauti zao zilianza kujitokeza kuhusu mwelekeo wa kisiasa na namna ya kushughulikia changamoto za kiuchumi za Senegal.

Kwa upande wake, Sonko ametangaza kuwa chama cha PASTEF hakitashiriki katika serikali mpya, akieleza kuwa bado kuna tofauti kubwa kati yake na Rais.

Licha ya kuondolewa katika nafasi ya waziri mkuu, Sonko bado ana ushawishi mkubwa kisiasa. Hivi karibuni alichaguliwa kuwa Spika wa bunge na anaendelea kuongoza chama cha PASTEF, chama chenye viti 130 kati ya 165 bungeni. Hali hiyo inampa uwezo mkubwa wa kusimamisha na hata kuzuia baadhi ya mipango ya serikali ya Faye.

Mgogoro huu unatokea wakati Senegal ikikabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi.

Deni la taifa limefikia takriban asilimia 132 ya pato la taifa (GDP) baada ya kubainika kuwa madeni ya awali yalikuwa yameripotiwa chini ya kiwango halisi.

Kutokana na hali hiyo, Shirika la Fedha la Kimataifa lilisimamisha mpango wake wa mkopo wa Dola bilioni 1.8 kwa Senegal. Wachambuzi wanaonya kuwa mvutano kati ya Faye na Sonko unaweza kufanya mazungumzo yajayo na Shirika la Fedha la Kimataifa kuwa magumu zaidi na kuchelewesha mageuzi muhimu ya kiuchumi.

CHANZO:AFP
Soma zaidi
Maambukizi ya Ebola DRC yaongezeka hadi 282, serikali imesema
Mahakama ya usuluhishi yakataa madai ya Dola milioni 134 ya Rwanda kwa mkataba wa Uingereza
Mamia waandamana nje ya kituo cha karantini cha Ebola cha Kenya kwa raia wa Marekani
Maombolezi yaendelea kwa wanafunzi 16 waliokufa moto shuleni Kenya huku lawama zikienea
Wapiga kura wajitokeza kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu nchini Ethiopia
Wagonjwa watano wapona Ebola nchini DRC, WHO yathibitisha
Mkuu wa WHO ahimiza mazishi salama huku mlipuko wa Ebola DRC ukiendelea kukua
Mlipuko wa Ebola katika DRC unazidi juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo : MSF
RSF ya Sudan yaua raia 27 katika mashambulizi dhidi ya vijiji vya Kordofan Kaskazini
Zambia yathibitisha hakuna maambukizi ya Ebola kwa walioshukiwa kuvuka mpaka
Marekani bado yakazia macho kituo cha Ebola kilichopendekezwa nchini Kenya
Marekani yatuma vifaa vya kijeshi vya thamani ya $2.3M kwa Niger licha ya uhusiano mgumu
Saudi Arabia yatangaza kumalizika kwa ibada ya Hajj huku  mahujaji wakifika milioni 1.7 mwaka 2026
Familia ya aliyekuwa Rais wa Zambia Lungu yaelekea Mahakama ya Rufani kutokana na mzozo na serikali
Wanafunzi 8 nchini Kenya washikiliwa na polisi kufuatia ajali ya moto katika shule ya wasichana
WHO yatangaza mgonjwa wa kwanza kupona mlipuko wa Ebola DRC
Maafisa wa uhamiaji Marekani washtumiwa kwa kumtesa raia wa Ghana aliyekuwa mjamzito
Mahakama ya Kenya yasitisha kwa muda mpango wa kituo cha karantini cha Marekani nchini humo
Kituo cha Afya Afrika kinalenga kupata chanjo ya Ebola kufikia mwishoni mwa 2026
Kenya yaidhinisha kituo cha Marekani kwa karantini ya Ebola kutokana na mlipuko DRC, afisa asema