Mataifa matano Afrika yakabiliana na milipuko ya polio, lakini mapambano bado yanaendelea
AFRIKA
3 dk kusoma
Mataifa matano Afrika yakabiliana na milipuko ya polio, lakini mapambano bado yanaendeleaBurundi — pamoja na Ghana, Guinea-Bissau, Jamhuri ya Congo, na Uganda — zimefanikiwa kuzuia maambukizi ya virusi vya polio, kuashiria hatua muhimu kwa safari ya Afrika katika kuangamiza ugonjwa huo.
Juhudi za kutoa chanjo na uchunguzi katika maeneo mbali mbali zimesaidia kukinga watoto kutokana na polio. Picha: Unicef

Wakati wahudumu wa afya nchini Burundi walipogundua kuwepo kwa mlipuko wa virusi vya polio Machi 2023, taarifa hizo zilishtusha kote katika kanda ambazo awali zilitangazwa kutokuwa tena na maradhi ya polio miaka mitatu iliyotangulia.

Virusi hivyo, ambavyo vinaweza kusababisha kupooza kabisa huathiri watoto walio na umri chini ya miaka mitano, kutatiza mafanikio ya miongo kadhaa ya kukabiliana na virusi hivyo.

Miaka mitatu baadaye, Burundi — pamoja na Ghana, Guinea-Bissau, Jamhuri ya Congo, na Uganda — zimefanikiwa kuzuia maambukizi ya virusi vya polio, kuashiria hatua muhimu kwa safari ya Afrika katika kuangamiza ugonjwa huo.

Kufuatia tathmini ya kuhakiki kati ya mwezi Januari na Juni 2026, ilibainika kuwa maambukizi yalikabiliwa katika nchi zote tano. Ofisi ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani ilitangaza kumalizika kwa milipuko ya virusi vya polio.

Muktadha tofauti, mikakati ya pamoja

Hakuna tiba ya polio lakini kuna kinga kupitia chanjo salama.

Nchini Burundi, mamlaka za afya zimeongeza juhudi za chanjo na vipimo kwa usaidizi wa GPEI. Kuhamasisha chanjo, kuimarisha vipimo, kumesaidia kupunguza maambukizi na kulinda watoto kutokana na polio.

Tahadhari dhidi ya kubweteka

Licha ya mafanikio hayo, wataalamu wa afya wanaonya dhidi ya kubweteka. Hatari ya virusi vya polio kurudi tena ni wazi — kama ilivyobainika hivi karibuni nchini Madagascar kufuatia kutangazwa kumalizika kwa mlipuko hapo awali.

Kote barani Afrika, kuligunduliwa maambukizi zaidi ya 180 ya polio mwaka 2026 pekee, huku idadi kubwa ikiwa katika eneo la Ziwa Chad na Pembe ya Afrika.

Duniani, Afghanistan na Pakistan ndiyo nchi pekee ambazo zina maambukizi hatari ya virusi vya polio.

Mawaziri wa afya barani Afrika hivi karibuni waliidhinisha mpango wa miaka 10 wa juhudi za kuangamiza polio kwa kuimarisha mifumo ya afya kote barani Afrika. Mpango huo ni wa Shirika la Afya Duniani, Kanda ya Afrika 2026–2035.

"Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kukabiliana na polio Afrika kunahitaji utashi kutoka kwa nchi, ufadhili wa fedha na kujumuisha mikakati ya polio kwenye mfumo mzima wa afya," anasema Dkt. Mohamed Gedi, Mratibu wa Mpango wa Kuangamiza Polio wa Shirika la Afya Duniani, Kanda ya Afrika anasema. "Kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wenye kinga, uchunguzi zaidi na kujiandaa dhidi ya milipuko, tunaweza kuwa na hali ya kutokuwa na polio na kuimarisha hali yetu ya afya kote barani."

Dkt. Mohamed Janabi, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, Kanda ya Afrika, anaunga mkono hoja hii: "Pamoja na kuwa ni hatua muhimu, bado hatutakiwi kubweteka. Kuendeleza uchunguzi, kuwa makini na kuhakikisha chanjo inafikia watu wengi bado ni muhimu kuwalinda watoto na kuepuka milipuko katika siku za baadaye."

CHANZO:TRT Afrika English