Kocha maarufu wa Manchester City, Pep Guardiola, ametangaza rasmi kuwa ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu wa 2025/26, akihitimisha kipindi cha miaka 10 kilichojaa mafanikio makubwa katika soka la England na Ulaya.
Tangazo hilo limehitimisha enzi moja ya kipekee ambapo Guardiola ameifanya Manchester City kuwa moja ya timu bora zaidi duniani, akishinda jumla ya takribani vikombe 20 katika mashindano mbalimbali, ikiwemo Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Guardiola ameeleza kuwa uamuzi wake haukutokana na mgogoro wowote, bali ni wakati wake wa kuondoka: “Usiniulize sababu za kuondoka. Hakuna sababu maalum. Ndani yangu najua ni kuwa wakati wangu umefika.”
Aliongeza kuwa, “Hakuna kitu cha kudumu milele. Kama kingekuwa, ningebaki hapa.”














