Hawa ndio wagombea wa urais Rwanda 2024
Kampeni zimepamba moto nchini Rwanda. Wagombea watatu wa kiti cha urais wameanza kampeni katika sehemu tofauti za nchi kwa lengo la kuuza sera ili kuwashawishi wananchi kuwapigia kura katika uchaguzi mkuu wa 15 Julai 2024. Rais Paul Kagame ambaye ameongoza Rwanda tangu 2000 anawania kiti tena . Katika kinyang'anyiro hicho pia kuna Frank Habineza na Philippe Mpayimana ambao wamewahi kuwania tena kiti cha urais na kushindwa.