| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki ipo tayari kiusalama kuelekea mkutano wa NATO
Mamlaka nchini humo, zimekamilisha mapitio kiusalama wa viwanja vya ndege, kumbi za mikutano, na barabara mbalimbali kama viongozi kuingia jijini Ankara.
Uturuki ipo tayari kiusalama kuelekea mkutano wa NATO
Kulingana na Ciftci, vikosi vya ulinzi na usalama vitaendelea kufanya kazi kwa ukaribu kuhakikisha kuwa Uturuki inabaki salama wakati wote./Picha:AA / AA

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Mustafa Ciftci amesema kuwa mamlaka za nchi hiyo zimekamilisha maandalizi ya kiusalama kuelekea mkutano wa 36 wa NATO.

Kupitia ujumbe wake uliowekwa kwenye mtandao wa X siku ya Jumatatu, Ciftci alibainisha kuwa, aliendesha kikao ndani ya wizara hiyo, kwa lengo la kupitia hali ya kiusalama, kuelekea mkutano wa siku mbili wa viongozi wa NATO, ambao unaanza siku ya Jumanne jijini Ankara.

Kulingana na Ciftci, huli ni tukio la kihistoria kwa Uturuki.

“Mafanikio haya yanatokana na uongozi thabiti wa Rais Recep Tayyip Erdogan, na utayari wake wa kukuza amani na demokrasia, na nafasi ya Uturuki kimataifa,” alisema Ciftci.

“Jukumu letu ni kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa, hasa katika eneo la ulinzi na usalama,” aliongeza.

“Tumeangazia maeneo mbalimbali yenye kuhitaji usalama wa hali ya juu, kama vile hoteli, viwanja vya ndege, usalama wa mtandao, barabara na viashiria vingine vya hatari,” alieleza waziri huyo.

Kulingana na Ciftci, vikosi vya ulinzi na usalama vitaendelea kufanya kazi kwa ukaribu kuhakikisha kuwa Uturuki inabaki salama wakati wote wa mkutano huo.

CHANZO:AA