| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Watu 17 wafa maji nchini Libya
Inaripotiwa kuwa, boti hiyo ilikuwa inaelekea nchini Ugiriki, ikitokea katika mji wa Tobruk, ulioko Mashariki mwa Libya, kabla ya kuzama, umbali wa kilomita 100 kutoka Tobruk.
Watu 17 wafa maji nchini Libya
Inaripotiwa kuwa, boti hiyo ilikuwa inaelekea nchini Ugiriki, ikitokea katika mji wa Tobruk, ulioko Mashariki mwa Libya kabla ya kuzama./Picha:Wengine

Boti iliyokuwa imebeba wahamiaji 33 kutoka Sudan, imezama katika bahari ya Mediterania mashariki mwa Libya na kuua watu 17, huku wengine tisa wakiwa hawajulikani walipo.

Kulingana na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), watu saba kati ya hao, waliokolewa katika ajali hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM), watu hao walikutwa wakiwa peke yao baharini, huku wengine wakipoteza maisha kwa kukosa chakula na maji ya kunywa.

Inaripotiwa kuwa, boti hiyo ilikuwa inaelekea nchini Ugiriki, ikitokea katika mji wa Tobruk, ulioko Mashariki mwa Libya, kabla ya kuzama, umbali wa kilomita 100.

Kulingana na IOM, shughuli za uokozi, zilifanywa pamoja na jeshi la maji la Libya pamoja na taasisi zingine.

CHANZO:AP