| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki yakana madai ya kuingilia siasa za ndani za Somalia
Katika taraifa yake ya Jumatano iliyowekwa kwenye mandao wa kijamii wa Uturuki unaofahamika kama NSosyal, serikali ya nchi hiyo imeziita taarifa hizo kuwa ni “potofu na zilizokosa ukweli."
Uturuki yakana madai ya kuingilia siasa za ndani za Somalia
Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zimedai kuwa Uturuki inatumia uwepo wa ngome yake ya kijeshi nchini Somalia./Picha:Wengine / Others

Serikali ya Uturuki imekana madai kuwa inaingilia siasa za ndani za Somalia, kama ilivyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zimedai kuwa Uturuki inatumia uwepo wa ngome yake ya kijeshi nchini Somalia, kushawishi baadhi ya wanasiasa nchini humo.

Katika taarifa yake ya Jumatano iliyowekwa kwenye mandao wa kijamii wa Uturuki unaofahamika kama NSosyal, serikali ya nchi hiyo imeziita taarifa hizo kuwa ni “potofu na zilizokosa ukweli."

Kulingana na taarifa hiyo, kwa muda mrefu sasa, Uturuki imedumisha ushirikiano wake wa kweli na halali na serikali ya shirikisho ya Somalia, kwa kuzingatia sheria za kimataifa zenye kulenga kuimarisha usalama na utulivu wa Somalia.

"Uwepo wa majeshi ya Uturuki nchini Uturuki unalenga kulifanyia mageuzi Jeshi la taifa la nchi hiyo na kuboresha mapambano dhidi ya ugaidi," taarifa hiyo ilisema.

CHANZO:AA