| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Watu wasiopungua 14 wauawa Sudan Kusini katika tukio la wizi wa ng'ombe
Watu wasiopungua 14 wameuawa, ikiwemo watoto sita, katika tukio la wizi wa ng'ombe kaskazini mwa Sudan Kusini, afisa wa eneo hilo alisema siku ya Jumatano.
Watu wasiopungua 14 wauawa Sudan Kusini katika tukio la wizi wa ng'ombe
Wizi wa ng’ombe kaskazini mwa Sudan Kusini umesababisha watu wasiopungua 14 kuuawa, maafisa wa eneo hilo wamesema Juni 3, 2026. / Reuters

Watu wasiopungua 14 wameuawa, ikiwemo watoto sita, katika tukio la wizi wa ng’ombe kaskazini mwa Sudan Kusini, afisa mmoja wa eneo hilo ameiambia AFP siku ya Jumatano.

Shambulio hilo lilitokea Jumanne usiku eneo la Padang Payam Jimbo la Unity.

"Kumekuwa na mashambulizi ya vijana wenye silaha kutoka eneo la Ruweng, na waliwaua watu wasiopungua 14 asubuhi hii, ikiwemo watoto sita, wanaume sita, mwanamke mmoja na msichana mmoja," Waziri wa Habari wa Jimbo la Unity Nyakenya Johannes Keah alisema, akiongeza kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.

Ng’ombe karibu 200 waliibiwa wakati wa shambulizi hilo na kupelekwa Ruweng, aliongeza.

Taarifa zinaonya mashambulizi zaidi jimbo la Jonglei

Waziri wa habari katika eneo la Ruweng, Salva Nyok, alikanusha madai hayo katika mawasiliano kwa njia ya simu na AFP.

Taarifa ya usalama kutoka Jumatatu, ambayo ilishuhudiwa na AFP, ilionya kuwa vijana walikuwa wanahamasishwa kuiba ng’ombe katika jimbo la Jonglei, ambako kumekuwa na mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na upinzani.

"Pamoja na kuwa lengo lilotajwa ni wizi wa ng’ombe, kuna hatari ya vurugu kuendelea zaidi ya wizi huo na kujumuisha wanasiasa na masuala ya kijamii," taarifa hiyo ilisema.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Marekani yawawekea vikwazo makamanda wanaohusishwa na vita mashariki mwa DRC
Uwanja wa ndege wa DRC katika eneo lilokumbwa na mlipuko wa Ebola wafunguliwa tena
Ghana yaonya raia wake kutosafiri Afrika Kusini kama hakuna ulazima
Wanafunzi tisa wafikishwa mahakamani Kenya kwa madai ya kuchoma moto shule
Serikali ya Tanzania inataka utatuzi wa haraka wa kero za watumishi wa umma
Rais Faye wa Senegal aunda serikali mpya bila chama cha Sonko
Mahakama Kuu Kenya yaendelea kuzuia mpango wa kujenga kituo cha Ebola
Maambukizi ya Ebola DRC yaongezeka hadi 282, serikali imesema
Mahakama ya usuluhishi yakataa madai ya Dola milioni 134 ya Rwanda kwa mkataba wa Uingereza
Mamia waandamana nje ya kituo cha karantini cha Ebola cha Kenya kwa raia wa Marekani
Maombolezi yaendelea kwa wanafunzi 16 waliokufa moto shuleni Kenya huku lawama zikienea
Wapiga kura wajitokeza kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu nchini Ethiopia
Wagonjwa watano wapona Ebola nchini DRC, WHO yathibitisha
Mkuu wa WHO ahimiza mazishi salama huku mlipuko wa Ebola DRC ukiendelea kukua
Mlipuko wa Ebola katika DRC unazidi juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo : MSF
RSF ya Sudan yaua raia 27 katika mashambulizi dhidi ya vijiji vya Kordofan Kaskazini
Zambia yathibitisha hakuna maambukizi ya Ebola kwa walioshukiwa kuvuka mpaka
Marekani bado yakazia macho kituo cha Ebola kilichopendekezwa nchini Kenya
Marekani yatuma vifaa vya kijeshi vya thamani ya $2.3M kwa Niger licha ya uhusiano mgumu
Saudi Arabia yatangaza kumalizika kwa ibada ya Hajj huku  mahujaji wakifika milioni 1.7 mwaka 2026