Kesi ya Bozize itasaidia kuponya vidonda vya Bossembélé, Jamhuri ya Afrika ya Kati?
AFRIKA
2 dk kusoma
Kesi ya Bozize itasaidia kuponya vidonda vya Bossembélé, Jamhuri ya Afrika ya Kati?Huku rais zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize akikabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, walionusurika mateso ya Bossembélé wanajiuliza maswali: kesi itakuwa na haki kama mshtakiwa hayupo?
Bozize, 79, alipindua serikali 2003 kabla ya yeye mwenyewe kuondolewa madarakani miaka 10 baadaye (AP Photo/Ben Curtis) / AP

Kesi ya Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) François Bozizé ilianza Juni 16 2026 mjini Bangui, kukiwa na matarajio inaweza kuwa moja ya hatua ya uwajibikaji nchini humo.

Na hata kabla ya ushahidi kuwasilishwa, swali ni: haki itapatikana kama kama mshukiwa mkuu yuko uhamishoni?

Mahakama hiyo maalum ya Umoja wa Mataifa (SCC) ilianza kesi yake kwa kumshtumu Bozize kwa kuhusika pakubwa na uhalifu dhidi ya ubinadamu unaodaiwa kufanyika kati ya 2009 na 2013.

Kwa waliouawa na walionusurika, kesi hii ni fursa ya kipekee ya kukabiliana na madhilia waliopitia katika historia ya nchi hiyo. Hata hivyo, kwa wasomi wa sheria na wanaharakati wa haki za binadamu, pia hili linaonesha tatizo la mfumo wa haki kimataifa: kuna mvutano kati ya kutafuta uwajibikaji na uhalali wa mchakato wenyewe.

Mzimu wa Bossembélé

Kuhusu Bossembélé, mji ulioko kilomita 150 kaskazini magharibi mwa Bangui ndipo waendesha mashtaka wanaeleza kuwa chimbuko la ugaidi uliofadhiliwa na serikali wakati wa utawala wa Bozize.

Wachunguzi wanadai kuwa raia walikamatwa kimakosa, kuteswa na kudhulumiwa gerezani na kambi za karibu za kijeshi. Waendesha mashtaka wanadai kuwa vurugu hizo zilikuwa sehemu ya mkakati wa serikali kubana upinzani na kutishia watu.

Maafisa wakuu wa jeshi wa zamani wanaohusishwa na madai ya dhulma hizo — Eugène Barret Ngaïkosset, Vianney Semndiro na Firmin Junior Danboy — bado wako gerezani na wanatarajiwa kushtakiwa mahakamani.

Bozize, mwenye umri wa miaka 79, ameishi uhamishoni Guinea-Bissau tangu Machi 2023 baada ya awali kuwepo nchi jirani ya Chad.

Hatua imepigwa lakini bado kuna maswali mengi

Licha ya utata uliopo, kesi hiyo ya SCC bado ni muhimu sana kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Inadhihirisha dhamira ya kukabiliana na baadhi ya zama za madhila katika nchi hiyo na kuonesha kuwa hata viongozi wa nchi hawawezi kukwepa mfumo wa sheria.

Whether the proceedings ultimately deliver justice, however, remains an open question.

Kwa walionusurika Bossembélé, kesi hii inatoa nafasi ya kutambuliwa kwa mateso waliopitia baada ya muda mrefu. Lakini kutambuliwa siyo sawa na kupatikana haki.

Huku majaji wakianza kupokea ushahidi mjini Bangui, kesi dhidi ya Francois Bozize inaonekana kuwa zaidi ya kumshtaki rais wa zamani. Ni kupima kama uwajibikaji unaweza kuwa na maana iwapo uhalali wenyewe unajadiliwa — na kama waliopatikana na madhila hayo wanaweza kupata suluhu mahakama ambayo watuhumiwa hawajafikishwa.

CHANZO:TRT Afrika