| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki yalenga kushirikiana na washirika wa NATO
Akizungumza wakati akiwakaribisha viongozi wa kutoka Jamhuri ya Czech, Albania, Romania, Croatia na Lithuania, Waziri wa Biashara wa Uturuki, Omer Bolat amesema kuwa Uturuki inaendelea kuongeza ujazo wa kibiashara kati ya Uturuki na Jamhuri ya Czech.
Uturuki yalenga kushirikiana na washirika wa NATO
Uturuki imeazimia kuimarisha ushirikiano wake na washirika wa NATO, wakati Ankara ikiwa mwenyeji wa Mkutano wa 36 wa viongozi wa NATO./Picha:AA / AA

Uturuki imeazimia kuimarisha ushirikiano wake na washirika wa NATO, wakati Ankara ikiwa mwenyeji wa Mkutano wa 36 wa viongozi wa NATO.

Akizungumza wakati akiwakaribisha viongozi wa kutoka Jamhuri ya Czech, Albania, Romania, Croatia na Lithuania, Waziri wa Biashara wa Uturuki, Omer Bolat amesema kuwa Uturuki inaendelea kuongeza ujazo wa kibiashara kati ya Uturuki na Jamhuri ya Czech, kwa lengo la kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi, hususani katika maeneo ya uwekezaji, viwanda, teknolojia na ulinzi.

Aliongeza kuwa, kwa kutumia nguvu ya kiuchumi ya Uturuki na eneo lake la kijiografia, Bolat alisema kuwa Uturuki itaendelea kuchangia kwenye ushirikiano wa kiuchumi na washirika wake.

Katika hatua nyingine, Bolat alisema kuwa, pia amemkaribisha Rais wa Croatia kwa ajili ya mkutano wa NATO.

Kulingana na Bolat, Uturuki na Croatia zinaendelea kudumisha ushirikiano wa, kwa manufaa ya mataifa hayo mawili.

Muda mfupi baadae, waziri huyo alimkaribisha Waziri Mkuu wa Albania, ambaye amefika nchini Uturuki kwa ajili ya Mkutano wa viongozi wa NATO.

CHANZO:َAA