“Mabaki ya ndege yalipatikana majira ya saa 3:15 asubuhi leo. Kwa bahati mbaya, hakuna walionusurika,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Desert Air, Willem de Wet, akifichua kuwa ndege hiyo ilikuwa imepotea tangu Jumapili.
“Tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia, marafiki, na wapendwa wa waliopoteza maisha yao katika ajali hii ya kusikitisha,” alisema, akiongeza kuwa ndugu wa marehemu walikuwa tayari wamearifiwa.
Kampuni ya Desert Air ilisema kuwa ndege aina ya Cessna 210 ilianguka baada ya kuondoka kwenye uwanja binafsi wa ndege karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, ikiwa inaelekea kwenye hoteli binafsi huko Sossusvlei, eneo linalojulikana kwa matuta yake makubwa ya mchanga yenye rangi ya udongo wa kahawia.
Uchunguzi umeanza
Kampuni hiyo ilisema uchunguzi umeanza ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Jangwa la Sossusvlei, ambalo ni kivutio maarufu cha watalii, lina eneo la chumvi na udongo mweupe ambapo miti iliyokufa ya Jangwa la Namib huonekana kana kwamba imegandishwa.
Picha ya eneo hilo hupatikana karibu katika kila kitabu cha mwongozo wa utalii kuhusu Namibia.
















