| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Mkenya Sabastian Sawe aweka historia marathon kwa kumaliza muda wa chini ya saa mbili
Sawe, akiwa na nia ya kuweka rekodi, aliongoza tangu mwanzo, na baadaye kumpita kwa umbali Kejelcha, na kisha kupanua wigo zaidi na kumaliza bingwa.
Mkenya Sabastian Sawe aweka historia marathon kwa kumaliza muda wa chini ya saa mbili
Mwanariadha wa Kenya Sebastian Sawe akimaliza mbio za marathon za London kwa wanaume, Aprili 26, 2026.

Mwanariadha wa Kenya Sabastian Sawe amevunja rekodi ya marathon ya muda wa chini ya saa mbili katika historia siku ya Jumapili alipomaliza mshindi katika mbio za London Marathon siku ya Jumapili.

Bingwa huyo mtetezi alikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mwanaridha wa Ethiopia Yomif Kejelcha lakini baadaye akampita kwa umbali na kumaliza katika muda wa saa 1 dakika 59 na sekunde 30.

Kejelcha pia alimaliza chini ya saa mbili, muda wake ukiwa 1:59:41, huku mwanariadha wa Uganda Jacob Kiplimo akiwa wa tatu (2:00:28).

Wote watatu wameipiku rekodi ya dunia ya mbio za marathon kwa wanaume ya 2:00:35 iliyowekwa Chicago 2023 na marehemu Kelvin Kiptum.

Mkenya Eliud Kipchoge alimaliza marathon katika muda wa 1:59:40 mwezi Oktoba 2019, na kuwa mtu wa kwanza kabisa katika historia kumaliza chini ya muda wa saa mbili.

Lakini muda huo haukusajiliwa kama rekodi ya dunia kwa sababu alikuwa na viatu maalum vya kumsaidia, pia utaratibu wa mashindano haukuzingatiwa kikamilifu, na hazikuwa mbio za ushindani.

Sawe, ambaye alivaa viatu vya Adidas Pro Evo 3, ambavyo uzito wake ni chini ya gramu 100, alidokeza kabla ya mbio za Jumapili kuwa lengo lake lilikuwa kuweka rekodi ya London au hata rekodi ya dunia.

CHANZO:TRT Afrika Swahili