| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Kiwanda cha mafuta cha Dangote Nigeria chaongeza uwezo, chasafisha mapipa 700,000
Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote hivi karibuni kimekuwa msambazaji mkubwa huku kukiwa na tatizo la bidhaa hiyo kutokana na mgogoro Mashariki ya Kati.
Kiwanda cha mafuta cha Dangote Nigeria chaongeza uwezo, chasafisha mapipa 700,000
Kiwanda hicho, kinachomilikiwa na bilionea Aliko Dangote, kilianza uzalishaji 2024. / Wengine

Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Nigeria cha Dangote kimeongeza uwezo hadi mapipa 700,000 kwa siku wakati wa majaribio.

Hii ni zaidi ya uwezo wake wa awali wa mapipa 650,000 kwa siku, ikiwa ni hatua kubwa zaidi.

Makamu wa Rais wa Mafuta na Gesi wa katika kiwanda cha Dangote, Devakumar Edwin, alisema siku ya Alhamisi, Juni 4, kiwango hicho ni mpango wa kuongeza uwezo wa hadi mapipa milioni 1.4 katika kipindi cha miezi 30 ijayo.

Ikifanikiwa, kiwanda cha Dangote kitakuwa moja ya viwanda vikubwa duniani.

Kiwanda hicho, kinachomilikiwa na bilionea Aliko Dangote, kilianza shughuli zake za mafuta mwaka 2024 baada ya miaka kadhaa ya ujenzi uliogharimu dola bilioni 20.

Usambazaji nchini na kimataifa

Tangu wakati huo imeongeza uzalishaji wake wa petroli, dizeli, na mafuta ya ndege. Inasambaza katika soko la nyumbanina kuuza nje kwa mataifa ya Kiafrika na Ulaya, ikiwemo Uingereza, Ufaransa na Uholanzi. Pia inapeleka baadhi ya bidhaa Marekani na Saudi Arabia.

Mapema siku ya Jumanne, Juni 2, Afisa Mkuu Mtendaji wa kiwanda hicho, David Bird, alisema katika mkutano na waandishi wa habari London kuwa kiwanda hicho kina mafuta zaidi ya ndege na kinaweza kusambaza bidhaa hiyo "kote duniani".

Aliongeza kuwa kiwanda hicho kinalenga kusafisaha mapipa 700,000 kwa siku "kufikia mwisho wa mwaka 2028".

Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote hivi akriubuni kimekuwa msambazaji mkubwa huku kukiwa na tatizo la bidhaa hiyo kutokana na mgogoro Mashariki ya Kati.

CHANZO:TRT Afrika and agencies