| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Kenya yaruhusu matumizi ya ‘mafuta machafu’ kukabiliana na uhaba wa mafuta duniani
Kulingana na Wizara ya Biashara ya nchi hiyo, mafuta yaliyo chini ya kiwango yatatumika kwa kipindi cha miezi sita.
Kenya yaruhusu matumizi ya ‘mafuta machafu’ kukabiliana na uhaba wa mafuta duniani
Serikali ya Kenya imeamua ‘kulainisha’ sheria zake na kuruhusu matumizi ya mafuta yaliyo chini ya kiwango./Picha:Wengine

Serikali ya Kenya imeamua ‘kulainisha’ sheria zake na kuruhusu matumizi ya mafuta yaliyo chini ya kiwango, katika kukabiliana na upungufu wa nishati hiyo, kufuatia vita vya Iran.

Kulingana na Wizara ya Biashara ya nchi hiyo, mafuta yaliyo chini ya kiwango yatatumika kwa kipindi cha miezi sita.

“Ombi la wizara ya nishati na huduma za petroli la kuongeza matumizi ya kemikali za salfa hadi kufikia kiwango cha ukomo wa miligramu 50 kwa kilo kwa kipindi cha miezi 6, limekubaliwa na wizara ya uwekezaji, biashara na viwanda,” ilisomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na wizara hiyo siku ya Alhamisi.

Hatua hiyo, inalenga kuwezesha upatikanaji wa nishati ya mafuta wakati wote na kuimarisha uchumi wa nchi hiyo, kadiri mgogoro wa Mashariki ya Kati utakavyoendelea, ilisema wizara hiyo.

Kwa kiasi kikubwa, Kenya inategemea bidhaa za mafuta kutoka nchi za guba, na ni kati ya nchi zilizoathirika zaidi toka kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz.

Siku ya Alhamisi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alitadhaharisha kuwa, kuendelea kufungwa kwa mlango huo, kutaendelea kuathiri uchumi wa dunia, na itachukua muda mrefu kurudi katika hali yake ya kawaida.

CHANZO:AFP