Anthony Joshua ametia saini kwa ajili ya pambano la ngumi dhidi ya bingwa mwenzake wa zamani wa uzani wa juu Tyson Fury, promota wa ndondi Eddie Hearn ametangaza.
Joshua, ambaye hajapigana tangu kupata ajali mwezi Disemba, kwanza atapambana na Kristian Prenga mjini Riyadh, Saudi Arabia, Julai 25.
Fury na Joshua - ambao wote wamepata ubingwa mara mbili - ni Waingereza, lakini hakujakuwa na pambano kati yao.
Joshua, 36, inabidi kwanza ashinde shindano lake la ngumi dhidi ya Prenga, raia wa Albania mwenye umri wa miaka 35 - ambaye ameshinda mara 20, ushindi wote kwa kuangusha mpinzani, na amepoteza pambano moja pekee.
Pambano la hivi karibuni la bondia huyo wa Uingereza lilikuwa dhidi ya Jake Paul mwezi Disemba.
Baadaye mwezi huo dereva wa Joshua alipata ajali nchini Nigeria, na kusababisha vifo vya watu wawili walio kwenye timu ya ndondi ya Joshua.
Tarehe ya pambano hilo la Anthony Joshua na Tyson Fury mwenye umri wa miaka 37 bado haijatangazwa.

















