| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Ronaldo na Messi Kombe la Dunia mara ya 6
Kuna Kombe la Dunia alafu kuna Messi wengine wanamuita ‘Andunje.’ Kuna Kombe la Dunia 2026 alafu kuna mkali wa hizi kazi, Ronaldo.
Ronaldo na Messi Kombe la Dunia mara ya 6
Cristiano Ronaldo. / Reuters

Ronaldo na Messi wanashiriki michezo hii kwa mara ya sita ikiwa wote walianza mwaka 2006 walipokuwa makinda pale Ujerumani.

Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro mzaliwa wa mji wa Madeira, Ureno ana umri wa miaka 41 naye Lionel Andres Messi wa Argentina akiwa na umri 38.

Wameshinda mataji mengi katika majukwaa mbalimbali na Messi amefanikiwa kunyanyua hadi Kombe la Dunia 2022.

Ronaldo hajafanikiwa hilo, lakini ameweka wazi mashindano yatakuwa ya mwisho kwake, licha ya kocha wake Roberto Martinez kusema kuwa anaweza kucheza hata akiwa na umri wa miaka 45.

2030 Ureno ni mwenyeji mwenza pamoja na Morocco na Hispania.

Ronaldo anahitaji kulibeba kombe hili ili akamilishe safari yake ya soka na wakati akijiandaa alieleza kupitia mtandao wa kijamii akiandika kwa Kireno "Começa a Missão Mundial!’’ maana yake ‘’Kampeni ya Kombe la Dunia imeanza’.’

Lionel Messi sasa hivi anacheza soka nchini Marekani, na makali yake yako pale pale akiwa na imani kuwa watatetea ubingwa wao.


Kufikia sasa, Ronaldo ndiye mwenye magoli mengi zaidi katika soka akiwa na jumla 970, ana nia ya kutimiza 1,000 kabla ya kutundika daluga.

Je, Ureno ya Ronaldo itafanikisha azma yake ya kuchukua ubingwa wa Kombe la Dunia?

 

CHANZO:TRT Afrika Swahili