| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Sudan yafuta vyeo vya juu vya kijeshi
Mabadiliko hayo yanafanyika huku kukiwa na mgogoro kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF, ulioanza toka mwaka 2023.
Sudan yafuta vyeo vya juu vya kijeshi
Jeshi la nchi hiyo limesisitiza kuwa maofisa watakaoathirika na maamuzi hayo, watabakia kuwa maofisa wa kawaida ndani ya jeshi la Sudan./Picha:Wengine
tokea masaa 2

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan, Abdel Fattah al-Burhan amepitisha azimio litakalo ondoa vyeo vya kijeshi nchini humo.

Kulingana na jeshi la nchi hiyo uamuzi huo unalenga kuondoa vyeo vya Naibu Amiri Jeshi Mkuu na wasaidizi wa kiongozi wa kijeshi wa Sudan.

Jeshi la nchi hiyo limesisitiza kuwa maofisa watakaoathirika na maamuzi hayo, watabakia kuwa maofisa wa kawaida ndani ya jeshi la Sudan.

Mwezi Mei mwaka 2023, al-Burhan alimteua Shams al-Din Kabbashi kama naibu kamanda, huku pia, akiwateua Yasser al-Atta na Ibrahim Jaber kama wasaidizi wa Amiri Jeshi Mkuu.

Mabadiliko hayo yanafanyika wakati kukiwa na mgogoro kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF, ulioanza toka mwaka 2023.