Muigizaji wa Marekani RJ Mitte, anayejulikana zaidi kwa uhusika wake katika tamthilia maarufu ya televisheni ya Breaking Bad, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 34.
Mitte aliigiza kama Walter White Jr., mwana wa mhusika aliyechezwa na Bryan Cranston, Walter White—mwalimu wa kemia anayekuja kuwa kinara wa biashara ya dawa za kulevya. Alionekana katika misimu yote mitano ya tamthilia hiyo, ambayo ilihitimishwa mwaka wa 2013.
Msimamizi wake alithibitisha kifo chake huku akisema kuwa alijitoa uhai mwenyewe.
Cranston alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutuma rambirambi zake kwa familia ya Mitte huku akitaja kifo ckake kama pigo kubw akwake binafsi na kwa ulimwengu wa sanaa.
‘‘Nimejawa na huzuni kubwa kufuatia kifo cha Mitte. Nakumbuka kukutana naye akiwa na umri wa miaka 14 tu, wakati muigizaji huyo kijana alipochaguliwa kuigiza kama mwanangu. Kweli alikuwa na azma katika kukabiliana na changamoto za ugonjwa wa mtindio wa ubongo (cerebral palsy) huku akimudu mahitaji ya kazi ya uigizaji.’’ aliandika Cranston.
Kwa kuwa alizaliwa na ulemavu wa cerebral palsy, Mitte alitumia uzoefu wake binafsi kuigiza uhusika huo, jambo lililosaidia kuongeza muonekano na utambuzi wa watu wenye ulemavu katika vyombo vikuu vya habari na televisheni.
Mbali na uigizaji, alikuwa mtetezi mashuhuri wa haki za watu wenye ulemavu; aliwahi kuwa balozi wa mashirika ya United Cerebral Palsy na Shriners Children's, na pia aliongoza taasisi ya Mitte Foundation.
Muigizaji mwenzake katika Breaking Bad Aaron Paul alisema kuwa "ameishiwa na maneno" na "amevunjika moyo," akimzungumzia Mitte kama rafiki aliyempenda na ambaye angemkumbuka sana. Pia alitumia ujumbe huo wa heshima kuwakumbusha watu wanaousoma kwamba wanapendwa na hawako peke yao.
Taarifa za kifo chake zilitolewa na wawakilishi wake siku ya Jumatatu, tarehe 12 Oktoba. Sababu ya kifo chake haijawekwa wazi rasmi.
Bryan Cranston, ambaye aliigiza kama baba yake katika tamthilia hiyo, alitoa salamu za rambirambi na kumzungumzia Mitte; alielezea kifo hicho kuwa pigo kubwa na kusifu azma yake, kipaji, pamoja na juhudi zake za kutetea wasanii wenye ulemavu.

















